Utani pembeni: Taifa stars kwa kwenda mbele, Afrika mashariki tuko nyuma yenu

Hilo ndio Tatizo la wakenya, wakifanya vibaya, utasikia hawataji Kenya wanatumia kivuli cha East Africa, ila wakifanya vizuri, hapo hamna East Africa, ni Kenya kwa kwenda mbele, mtanzania akifanya vizuri, basi huyo ni East Africa, ila wakifanya vibaya, hao ni watanzania. Huo ni ubinafsi wa wakenya uliokomaa sana.
 

Ni ukweli mchungu lakini lazima uukubali na kuumeza, kwenye mpira Afrika mashariki tuko ovyoo, hata hao Uganda hawaendi popote, watafungasha na kutufuata. Huu uzi nilianzisha bila kuegemea popote, hata kabla mechi hazijaanza, nilitegemea walau mojawapo wa hizi timu itafanya kitu cha kuonekana, ila tumeishia aibu tena kipigo kilichotoshana cha kila mmoja mabao mawili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…