Utani: UKUTA umefanyika ingawa si na walengwa. Hongereni watanzania wenzangu kwa amani yetu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
UKUTA ulitangazwa na CHADEMA. Watangazaji wakajipanga kimaandalizi bila ajizi. Wanasiasa,viongozi wa dini,wa kiserikali na walinzi wa amani wakajitokeza na kukataza. Wengine wakafanya mazoezi ya kujiandaa kukata mizizi. Wengine leo ni birthday yao na wanashereheka kivyao.

UKUTA ukazua mjadala,ubishani na kuwekwa kwenye mizani. Kadiri ulivyokuwa ukisisitizwa kuwepo leo,mikwara ya kauli kalikali ilizidi. Ukaahirishwa kupisha mazungumzo ya kusaka suluhu kuzama kwenye Safina ya NUHU.

Difenda zimerandaranda kama vinanda mitaani bila utani. Bado zinaendelea. Kiintelijensia,huko ni kuhakiki bila mikiki. Kuhakiki kama kauli ya jana si kanyaboya au hewa. Wapinga UKUTA wakajikuta wanaujenga UKUTA kuupinga UKUTA. Mwisho,UKUTA ukafanyika. Watanzania tujipongeze kutunza amani yetu. Yote yanazungumzika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Serikali imecheza mziki wa Chadema.
 

Vipi watani zako wanamtambua raisi wa Jamhuri au UKUTA unawazuia wasimuone na bado nchi iko mikononi kwa viongozi wa dini a.k.a washenga wa UKUTA. Mpongeze JPM kwa sherehe ya birthday.

Watanzania hawastahili pongezi kwa hili sababu wenyewe hawataki kuzuia hatari za kushika na kudondokewa na UKUTA.
 
Mkuu huu ni utani?, huu ni ukweli bana malengo ya UKUTA yamefikiwa kwa 99%
 
Hawa washika UKUTA wameanza kurudi kupitia mlango wa nyuma, jana walikimbia kabisa. UKUTA ungefanikiwa wasingetangaza kuuahirisha hadi oktoba mosi
 
Hongera CHADEMA kwa busara na upendo kwa mama Tanzania.
 
Nilikuwa sijasoma vizuri heading, kumbe unatania? wana wa UKUTA watakupopoa mawe.
 
ndiyo viongozi wa dini wanakwenda kuitafuta kwa rais?
Naam, kwa sababu bado hajajenga "chemistry" ya kuishi na upinzani, inabidi kwa sasa tutumie hao washenga ambao tunaamini kwamba ndio pekee anaowaheshimu kwa sasa
 
Hongera CHADEMA kwa busara na upendo kwa mama Tanzania.
Ningewashangaa kama wangeendelea na hatakati wakati Wanasikia Ndege angani. MBOWE kiboko anakuja na swaga eti viongozi wa dini wamemuomba, yeye nani?
 
Naam, kwa sababu bado hajajenga "chemistry" ya kuishi na upinzani, inabidi kwa sasa tutumie hao washenga ambao tunaamini kwamba ndio pekee anaowaheshimu kwa sasa
Mfalme wenu si alisema hawaheshimu?
 
Ukiona kiongozi wa polisi amesifia jambo upinzani bila kulazimishwa jua hali ilikua mbaya sana kwa upande wao. Kamanda Sirro" Nawasifu sana viongozi wa chadema kwa uzalendo wao wa hali ya juu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…