Utani wa Jadi unapogeuka uadui, Simba na Yanga ni Janga lijalo kwa Taifa letu

mzee wa bwaksi

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,255
Reaction score
3,972
Kwa miaka nenda rudi tumekuwa tukifurahia huu utani wa timu zetu pendwa Simba na Yanga Kwa amani tele.. Ila Ile amani kwa Sasa imetoweka kabisaa, Sasa umekuwa ni uadui na chuki kabisa miongoni mwa washabiki wa timu hizi. Imefikia hatua mtu akimuona mshabiki wa timu tofauti na anayoshabikia yeye anamuona kama tahaira/mjinga/mpumbavu fulani hivi.

Sasahivi lugha ya kutaniana imebadilika na kuwa lugha ya matusi ya nguoni, kejeli, dhihaka nk.
Ugomvi na mitafaruku mingi imetapakaa kila mahala kisa huu Usimba na Uyanga.
Imefikia hatua hadi watu wanaombeana mabalaa kisa tu ni huu huu uSimba na uYanga.

Kile kitu ambacho kilikuwa kikituunganisha kama taifa na kutupa furaha kama taifa Sasa ndicho kinatugawa Kwa kasi sana.

Viongozi wa mpira, viongozi wa serikali na washikadau wote wapo kimya kwa huu uadui na chuki zinazoshamili kwny Jamii yetu kisa tu u Simba na Yanga.
Waandishi wa habari nao pia wamekuwa sehemu ya kuendeleza uadui na chuki miongoni mwa washabiki wa timu hizi.

Kama taifa tuchukue hatua.

Huuu mpasuko ukiendelea kuachwa utakuja kutuletea shida huko mbeleni
 
Ajabu kweli kuona hili jambo linazungumzwa na shabiki wa Yanga.

Unataka mamlaka gani sasa ziingilie kati wakati mamlaka hizi hizi bado hamziheshimu na kila uchao mmekuwa mkizipiga vijembe?

Hizi mamlaka zikisema zianze utekelezaji wa hiyo hoja yako halafu ikatokea Yanga imekutwa na hatia na kisheria inapaswa kuwajibika si mtaandamana na kuzua utata zaidi ya huo kudai mamlaka zinawaonea nyie?

Ushauri wangu ni kwamba, hauhitaji mamlaka ili kukomesha tabia iliyopo ndani ya mtu (hususani shabiki)

Hata humu kuna members wana lugha zisizo za kiungwana kwa wengine kutokana na emotions za mpira.

Ni shabiki mwenyewe tu anapaswa kujitambua kwa kushare feelings na shabiki mpinzani, kujua hilo jambo analotaka kumfanyia mwenzake kabla hajalifanya ajaribu kulifikiria lingefanyika upande wake angejiskiaje. Ukishaona sio zuri basi kwanini umfanyie mwingine?
 
Mkuu nadhani hapa hukupaswa kunishambulia personal kisa ushabiki wangu kwa Yanga..
Hoja ni kuwa huu mpasuko ukiendelea kufumbiwa macho tutakuja kushuhudia makubwa huko mbeleni..
Binafsi nikupongeze kwa kuwa miongoni mwa wachangiaji wasiopenda kutumia lugha chafu humu jamvini tofauti na mashabiki wengi. Ila Kiukweli ushabiki wetu hivi Sasa umekuwa sio ushabiki Tena Bali ni uadui/ chuki/vita..
Tubadilike...
 
Mpira hoyeeeeee, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sikushambulii nakuelezea namna ulivyo

Otherwise leo utoke ku declare kwamba hufungamani na hizo mambo ambazo nimezianisha zinazofanywa na mashabiki wa Yanga

Ni mara ngapi humu mnaiita Simba TFF fc?

Sasa unavyosema mamlaka ziingilie kati na wakati huo mamlaka hizo hizo mnazidharau huoni kwamba huo ni unafki?

Mmetengeneza dhana mbaya sana kwa uongozi kuwa kila jambo litaloamuliwa ja mamlaka likawa na negative impact kwa Club yenu basi hiyo ni chuki ambayo mamlaka iko nayo dhidi yenu.

Badilikeni msiwe watu wakushikiwa akili na wapuuzi wachache, wapo wanaojielewa wamekaa mbali kwenye hili wakimuacha Manara alopoke kwasababu wanaelewa wapi Club ime messup, nyinyi mnaunga tela bila kujua kichwa kiko wapi ndio mnaopelekeshwa.
 
Kawaida sana.
Kama hutaki hayo Mambo usishabikie mpira.
 
Umeandika kwa hisia sana mpaka hueleweki unamlaumu nani.!
 
Kuna mtu alisema mashabiki kindaki ndaki wa hizi timu za Kariakoo wengi wao dishi limeyumba naanza kuamini.
 
Kuna mtu alisema mashabiki kindaki ndaki wa hizi timu za Kariakoo wengi wao dishi limeyumba naanza kuamini.
Ndio ndio mkuu.. Yaani Sasa imekuwa sio utani Tena bali ni matusi tupu. Sijui huu ni ustaarabu gani, tena na hizi fake ID's unaweza Kuta mtoto na mzazi wake wanatukanana matusi ya nguoni kabisaa
 
Kila kitu kimekua Simba vs Yanga. Napenda mpira but ushabiki wa kifala huu
Na ndio maana mambo ya msingiyanayohusu mstakabari wa maisha yao, hawana muda nayo kabisa!!yaani toka asubuhi hadi jioni ni kubishana mpira tu!!na vituo vyote vya radio siku hizi toka asubuhi ni vipindi vya mpira tu.Tz kwa kizazi hiki kuna safari ndefu sana.
 
Mwasisi wa chuki hizi ni Haji Manara. Mfano hai ni matusi na kejeli alizomporomoshea bondia Mwakinyo kwa vile ni tu Mwakinyo ni mshabiki wa Simba. Haji ni mtu hatari sana aonywe
 
Acheni kuumiza vichwa kwaajili ya Yanga na Simba,

Kama wewe

Hujaajiriwa Simba au Yanga,
Si mchezaji wa wa hizi club,

Fanya shughuli zingine
Tena mtuachie timu zetu sisi tunashindana na kukabiliana Kwa utani wa Hadi bila kusahau Tambo za hapana pale🤸🤸
 
Walitakiwa viongozi wa yanga waanzee kuwaambia mashabiki wao wasio jielewa kuacha kwenda kwenda kuwapokea wageni bila hvyo mimi kama naangalia mpira wa simba shabiki wa yanga anakuja kwetu kushangiria tukiwa tumefungwa si tuna mdunda tu kama nyinyi mlivyo wapiga coastal union arusha nataka siku shabiki wa utopolo ajichanganye mechi za simba lazima ajikute muhimbili nyie si mmeanzisha si tunamaliza.
 
Na yule nguruwe pori ndo anaharibu maana halisi ya utani wa jadi maana anasambaza sumu tu yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…