Pole sana mtoa mada. Hili tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria. Angalia mfano hapa, yaani Kwa vile tu mtoa mada ni Yanga washabiki wote wa Simba hawataki kujipa muda kufikiria mada wanamshambulia mtoa mada. Hii ni chuki kubwa sana.
Niliwahi kusema humu JF na nasema Tena, watanzania tunaenda kubaya Sana ni vile hatujui tu. Chuki inakuwa sehemu ya maisha yetu ya Kila siku, tazama Simba na Yanga, tazama CCM na upinzani(Chadema), tazama ukabila, tazama ukristo na uislam, tazama utanganyika na uzenji. Haya yote yanakuwa uadui wa waziwazi Sasa hivi ilhali zamani watu walivumiliana sana, waliishi Kwa Upendo regardless na kubeshimiana Sana
Simply sababu mawazo yametoka Kwa mtu wa Yanga basi Simba wote wanapinga na kumshambulia na nina Imani hata angeyatoa mtu wa Simba basi Yanga wangepinga.