Utani wa Makabila: Ijue Historia ya utani wa Makabila Tanzania

Lakini ulionaje? Si ilitoka pamoja na ukali wa Mkurya. Kama unataka nenda wewe ambaye siye mtani wa Mkurya ukafanye hivyo uje uone watakavyo kung'enta mapanga muraa!! Nakutema muraa!! Lakini sisi Wahaya na Wanyambo full kujidai kwa Mkurya na ananywea kabisaaaaa. Wajukuu wetu hawa hawana neno mnawaonea bure ni watoto wazuri
kuna jamaa angu mhaya alikua anaoa basi rafiki yetu mkurya akaenda pale kwenye kiti cha bwana harusi akakaa anagoma kutoka mpaka pesa itolewe
 
Wakurya ni wajukuu wa wahaya, kwa hiyo hata iwe vipi babu / bibi hawezi mdharau mjukuu. Na mjukuu hawezi chukizwa na utani wa babu/bibi.

Sie ni wajomba zao bwana, mhaya ni mpwa wetu watoto wa dada zetu
 
aaah karibu blaaza sukari ya warembo...mutu ya puturu.............. mutu ya minara kokonati oilii
 
Utani wa Wafipa na Wasukuma ni hatari
Wasukuma wana watani wangapi jamani...!? Pwani, Morogoro, Dodoma na Sasa Rukwa wote ni watani wa Wasukuma? Tunaomba chati inayoonyesha, kabila lipi lina taniana na lipi. Kwenye chati hiyo nitajua watani wangu wa ziada maana kijijini kwetu Kusadikika tunajulikana kwa kutania na akina Anduje Ngoswe Kibanga. Pia nilisikia Mgaramao na nao wanatatizwa na idadi ya makabila wanayotaniana nayo.
===
Asante sana mleta mada.
 
Wahehe vs wakirya
Waha vs wakurya
Wahaya vs wakurya
Wanyaturu vs wakurya
Wanyiramba vs wakurya
 
Wahehe vs wakirya
Waha vs wakurya
Wahaya vs wakurya
Wanyaturu vs wakurya
Wanyiramba vs wakurya
Duh! Wakurya nao wamebananishwa...Ha ha haa! Wakivamiwa na kundi lote hilo panakalika kweli. Ha ha aa!
 
Nawazaga ilitokeaje wasukuma wakawa na utani na wagogo na wazaramo na watu wote wa iringa? Kwanza wako mbalimbali kweli!!
 
Nafikiri ilikuwa ni strategical moves ya Nyerere kuwaunganisha watanzania na ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Kwani umewahi kusikia makabila ya jirani zetu waKenya ama kule Rwanda wakitaniana??
mhhh watu kumsifia nyerere vitu ambavyo hakufanya hamjambo ,utani ulikuwepu kabla nyerere hajazaliwa kenya pia makabila mengi yanautani nako ni nyerere hahahaha
 
"Wajeremani!"; "Wajeremani!"

Alisikika MC akiendelea kuita watani wa kabila la Wahehe.
 
Sikonge,
Eeenheee umeona utani ulivyo mkuu.
Imeandikwa kiutani utani na hata tumaneno ulitotumia kuwaponda Wangoni ni ya kiutani zaidi.
Mngoni alipofika kwetu Ipogolo joto la jiwe alikutana nalo.
 
Wakurya shida.
 
Prof Gwasa (RIP) wa UDSM alitoa andiko zuri sana kuhusu mada hii. Andiko lilichukua jina LA "Utani Complex". Ukitaka kujua zaidi kuhusu suala la utani kati ya makabila basis tafunta andiko hili.
 
Nafikiri ilikuwa ni strategical moves ya Nyerere kuwaunganisha watanzania na ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Kwani umewahi kusikia makabila ya jirani zetu waKenya ama kule Rwanda wakitaniana??
Wanataniana sana. Wajaluo na Wakalenjin, Waluo na waluhya nk
 
Utani kwa Tanzania huenda ni suala la kipekee, maana nchi nyingine husikii kuhusu utani. Sijawahi kusikia Kenya, Rwanda, Uganda, Burudi wala Zaire DR wana utani. Sijui labda upo.

Utani kwa Tanzania una miziz mirefu sana. Moja ya sababu zilizosababisha utani, ni kuoleana, vita, biashara na njia nyingine za mahusiano.

Waha kwa Tanzania ni kabila lenye idadi ya makabila mengi ambayo ni watani. Kila kabila lina historia anuwai ya chanzo cha utani. Baadhi ya makabila ambayo yana utani na waha ni makabila karibu yote ya mkoa wa Mara(kurya, jita, kerewe, kara), wahaya, wafipa, makabila karibu yote ya Tanga(digo, sambaa, bondei n.k), wangoni, sukuma n.k.

Chanzo cha utani wa muha na mngoni ni vita. Wangoni walisafiri hadi kufika Buha, makao makuu ya ufalme wa Buha. Wakaanzisha vita ili waliteke eneo hilo. Lakini walipata kipigo cha mbwa koko, wakatekwa na wakafanywa kuwa moja ya ukoo wa waha wakapewa jina la walengwe. Moja ya mambo yaliyofanywa na wangoni/walengwe, ni juhudi zao za kutafta maji pale buha. walianza kuunganisha mianzi waende kutoboa anga maji yamwagike. Hii ni akili mbovu ya mlengwe/mngoni. matokeo yake walikuwa wanaanguka na kufa, ndipo ikabaki historia ya AHAHELEYE ABHALENGWE yaani walipoteketea wangoni. Hadi leo eneo hilo lipo heru juu, au KUMGAZO ambapo baada ya kushindwa kutoboa anga, wakachimba handaki refu sana kwenda chini kutafta maji. Mpaka leo maeneo hayo yapo pale heru juu, wilaya ya Kasulu.

Chanzo cha historia ya Muha na Mfipa, ni vita pia. Lakini vita hii pamoja na kuingia vitani kwa kutumia zana mbalimbali, pia ni vita iliyohusisha mazingaombwe. Wafipa walitumia nyuki kuwadhibiti waha. Ndio maana hadi leo muha anaheshimiana na mfipa, ni wachawi sana. Na kila muha mchawi lazima ameenda kuomba uchawi kwa wafipa. Pia miaka ya 70 malkia wa mwisho wa Buha, Ntare inasemekana aliolewa na mtani wake mfipa. Ndio maana hawa jamaa ni watani.

Utani wa waha na makabila ya Tanga, ni kuoleana hasa baada ya manamba. Wahaasilimia kubwa walioenda Tanga kulima mkonge, hawakurudi buha, bali waliamua kuoa mabinti wa kitanga na kuamua kuishi huko. Kwa takwimu zisizo rasmi, waha ni moja ya kabila linalopatikana Tanga. Hivyo muha akimuona mtu waTanga, ni sawa amemuona mwanae. Ukiona mtu anajitambulisha mbondei, Mdigo, ukimchimba zaidi ni muha. Hta akina less/simba wanyika ni mazalia ya waha waliolowea hapo Tanga.

Utani wa muha na mkurya, mjita, mjaluo, kwa kiasi kikubwa ni watu waliotoka sehemu moja huko Africa Magharibi. Wana vitu vingi sana wanafanana. Yapo maeneo yaliyopo mara yanafanana kwakila kitu na maeneo ya Buha. Kimsingi hawa ni ndugu kama ilivyo kwa wahaya. Pia kuoleana kulisaidia.
 
Ha ha ha ha ha yote ni sawa la msingi wanaishi vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…