Utani wa Makabila: Ijue Historia ya utani wa Makabila Tanzania

Utani wa Makabila: Ijue Historia ya utani wa Makabila Tanzania

Sikonge,
Mkuu utasababisha uaminike umeandika fix. Bunduki hazikuwepo. Ni zana za chuma tu mkuki, upinde na mshale. Bunduki zimeletwa na wazungu.

Mngoni alipita kiulaini hapo tabora akaingia buha. Hadi leo wapo buha wanaitwa walengwe. walitandikwa wakasalimu amri kwa buha
 
Utani kwa Tanzania huenda ni suala la kipekee, maana nchi nyingine husikii kuhusu utani. Sijawahi kusikia Kenya, Rwanda, Uganda, Burudi wala Zaire DR wana utani. Sijui labda upo.

Utani kwa Tanzania una miziz mirefu sana. Moja ya sababu zilizosababisha utani, ni kuoleana, vita, biashara na njia nyingine za mahusiano.

Waha kwa Tanzania ni kabila lenye idadi ya makabila mengi ambayo ni watani. Kila kabila lina historia anuwai ya chanzo cha utani. Baadhi ya makabila ambayo yana utani na waha ni makabila karibu yote ya mkoa wa Mara(kurya, jita, kerewe, kara), wahaya, wafipa, makabila karibu yote ya Tanga(digo, sambaa, bondei n.k), wangoni, sukuma n.k.

Chanzo cha utani wa muha na mngoni ni vita. Wangoni walisafiri hadi kufika Buha, makao makuu ya ufalme wa Buha. Wakaanzisha vita ili waliteke eneo hilo. Lakini walipata kipigo cha mbwa koko, wakatekwa na wakafanywa kuwa moja ya ukoo wa waha wakapewa jina la walengwe. Moja ya mambo yaliyofanywa na wangoni/walengwe, ni juhudi zao za kutafta maji pale buha. walianza kuunganisha mianzi waende kutoboa anga maji yamwagike. Hii ni akili mbovu ya mlengwe/mngoni. matokeo yake walikuwa wanaanguka na kufa, ndipo ikabaki historia ya AHAHELEYE ABHALENGWE yaani walipoteketea wangoni. Hadi leo eneo hilo lipo heru juu, au KUMGAZO ambapo baada ya kushindwa kutoboa anga, wakachimba handaki refu sana kwenda chini kutafta maji. Mpaka leo maeneo hayo yapo pale heru juu, wilaya ya Kasulu.

Chanzo cha historia ya Muha na Mfipa, ni vita pia. Lakini vita hii pamoja na kuingia vitani kwa kutumia zana mbalimbali, pia ni vita iliyohusisha mazingaombwe. Wafipa walitumia nyuki kuwadhibiti waha. Ndio maana hadi leo muha anaheshimiana na mfipa, ni wachawi sana. Na kila muha mchawi lazima ameenda kuomba uchawi kwa wafipa. Pia miaka ya 70 malkia wa mwisho wa Buha, Ntare inasemekana aliolewa na mtani wake mfipa. Ndio maana hawa jamaa ni watani.

Utani wa waha na makabila ya Tanga, ni kuoleana hasa baada ya manamba. Wahaasilimia kubwa walioenda Tanga kulima mkonge, hawakurudi buha, bali waliamua kuoa mabinti wa kitanga na kuamua kuishi huko. Kwa takwimu zisizo rasmi, waha ni moja ya kabila linalopatikana Tanga. Hivyo muha akimuona mtu waTanga, ni sawa amemuona mwanae. Ukiona mtu anajitambulisha mbondei, Mdigo, ukimchimba zaidi ni muha. Hta akina less/simba wanyika ni mazalia ya waha waliolowea hapo Tanga.

Utani wa muha na mkurya, mjita, mjaluo, kwa kiasi kikubwa ni watu waliotoka sehemu moja huko Africa Magharibi. Wana vitu vingi sana wanafanana. Yapo maeneo yaliyopo mara yanafanana kwakila kitu na maeneo ya Buha. Kimsingi hawa ni ndugu kama ilivyo kwa wahaya. Pia kuoleana kulisaidia.
Kenya utani upo.......hasa wajaluo na Waluhya.......hadi derby yao ya mpira kati ya afc leopards(waluhya) na gormahia(luo) wanaiita mashemeji derby
 
Wakuu,

Nimezaliwa katika kizazi hiki cha dotcom na nikaikuta Tanzania ikiwa hai, ndani ya jamii ya nchi yetu hii nikakuta kuna muingiliano mkubwa wenye bashasha miongoni mwa wananchi. Ndani ya mipaka ya nchi hii ikajengwa hulka na tamaduni za kuondoleana utofauti kwa misingi ya dini, jinsia ukabila, ukanda n.k. Kinachonifanya kutafakari ni juu ya suala la Utani wa Makabila.
  • Je, ni nini kilikuwa chanzo cha kuanzisha utani wa kikabila (Mfano Wanyamwezi na Wagogo - WATANI)
  • Je, ni hali tuliyoirithi toka kwa wakoloni ama ilianza punde tulipopata uhuru?
  • Nani muanzilishi wa kutambulisha kabila hili ni watani wa kabila fulani?
  • Je, hali hiyo ya utani bado ipo mpaka leo na ikiwa hai au imebaki kuparurana tu?
  • Kwa wale mliokula chumvi nyingi, hali ya utani wa makabila ilijenga au lah!
Nawasilisha na naomba kusaidiwa kujuzwa ili niweze kufahamu juu ya hili, mniwie radhi iwapo nitakuwa nimeikosea jamii yetu kwa kuweka hoja hii mbele yenu.

----
BAADHI YA MICHANGO YA WANA-JF




CHANZO CHA UTANI WA WAHEHE NA WANGONI


Wangoni ndio kabila ambalo ni watani wa jadi wa Wahehe, moja ya sababu ambazo hutajwa kuwa sababu ya utani huu ni kuwa katika vita za kikabila zilizokuwa zikiendelea kabla ya ujio wa wakoloni, Wahehe na Wangoni waliwahi kupigana na hakukupatikana mshindi, na kuanzia hapo walianza utani kila moja akitamba kuwa bora kuliko mwenzie.

Utani wa makabila haya mawili ni utani wenye heshima watu wa rika moja ndio ambao hutaniana, hauhusishi matusi kama ulivyo utani wa baadhi ya makabila. Na utani huu hugeuka nyenzo muhimu ya kusaidiana wakati wa misiba ambapo watani husaidia kukusanya michango na kufanya kazi ambazo zinawapunguzia mzigo wafiwa.
Aisee hebu kacharaze vizuri bandiko lako ulitafutie nyama za kutosha kisha urejee hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je . Mtu anaweza kukwepa Mkono wa Sheria kwa kuvunja sheria ya kumtolea lugha ya kuudhi mwenzake kwa kisingizio cha Utani wa kikabila?

Swali kwenu wanasheria
 
Back
Top Bottom