Utani kwa Tanzania huenda ni suala la kipekee, maana nchi nyingine husikii kuhusu utani. Sijawahi kusikia Kenya, Rwanda, Uganda, Burudi wala Zaire DR wana utani. Sijui labda upo.
Utani kwa Tanzania una miziz mirefu sana. Moja ya sababu zilizosababisha utani, ni kuoleana, vita, biashara na njia nyingine za mahusiano.
Waha kwa Tanzania ni kabila lenye idadi ya makabila mengi ambayo ni watani. Kila kabila lina historia anuwai ya chanzo cha utani. Baadhi ya makabila ambayo yana utani na waha ni makabila karibu yote ya mkoa wa Mara(kurya, jita, kerewe, kara), wahaya, wafipa, makabila karibu yote ya Tanga(digo, sambaa, bondei n.k), wangoni, sukuma n.k.
Chanzo cha utani wa muha na mngoni ni vita. Wangoni walisafiri hadi kufika Buha, makao makuu ya ufalme wa Buha. Wakaanzisha vita ili waliteke eneo hilo. Lakini walipata kipigo cha mbwa koko, wakatekwa na wakafanywa kuwa moja ya ukoo wa waha wakapewa jina la walengwe. Moja ya mambo yaliyofanywa na wangoni/walengwe, ni juhudi zao za kutafta maji pale buha. walianza kuunganisha mianzi waende kutoboa anga maji yamwagike. Hii ni akili mbovu ya mlengwe/mngoni. matokeo yake walikuwa wanaanguka na kufa, ndipo ikabaki historia ya AHAHELEYE ABHALENGWE yaani walipoteketea wangoni. Hadi leo eneo hilo lipo heru juu, au KUMGAZO ambapo baada ya kushindwa kutoboa anga, wakachimba handaki refu sana kwenda chini kutafta maji. Mpaka leo maeneo hayo yapo pale heru juu, wilaya ya Kasulu.
Chanzo cha historia ya Muha na Mfipa, ni vita pia. Lakini vita hii pamoja na kuingia vitani kwa kutumia zana mbalimbali, pia ni vita iliyohusisha mazingaombwe. Wafipa walitumia nyuki kuwadhibiti waha. Ndio maana hadi leo muha anaheshimiana na mfipa, ni wachawi sana. Na kila muha mchawi lazima ameenda kuomba uchawi kwa wafipa. Pia miaka ya 70 malkia wa mwisho wa Buha, Ntare inasemekana aliolewa na mtani wake mfipa. Ndio maana hawa jamaa ni watani.
Utani wa waha na makabila ya Tanga, ni kuoleana hasa baada ya manamba. Wahaasilimia kubwa walioenda Tanga kulima mkonge, hawakurudi buha, bali waliamua kuoa mabinti wa kitanga na kuamua kuishi huko. Kwa takwimu zisizo rasmi, waha ni moja ya kabila linalopatikana Tanga. Hivyo muha akimuona mtu waTanga, ni sawa amemuona mwanae. Ukiona mtu anajitambulisha mbondei, Mdigo, ukimchimba zaidi ni muha. Hta akina less/simba wanyika ni mazalia ya waha waliolowea hapo Tanga.
Utani wa muha na mkurya, mjita, mjaluo, kwa kiasi kikubwa ni watu waliotoka sehemu moja huko Africa Magharibi. Wana vitu vingi sana wanafanana. Yapo maeneo yaliyopo mara yanafanana kwakila kitu na maeneo ya Buha. Kimsingi hawa ni ndugu kama ilivyo kwa wahaya. Pia kuoleana kulisaidia.