Utani wa Simba na yanga, kuhusu maandalizi ya timu

Mbobo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2017
Posts
1,392
Reaction score
1,818
MTANI UNATUANGUSHA SANA.

Simba: Andaeni Timu

Yanga: Mtakoma Chama kaondoka

Simba: Andaeni Timu

Yanga: Trh 28 kutakuwa na Suprise

Simba: Andaeni Timu

Yanga: Suprise ni Luis Miquissone.

Simba: Andaeni Timu msije kutulaumu

Yanga: Tumemchukua Msukule.

Simba: Msukule hatacheza andaeni Timu

Yanga: Subiri siku ya Wananchi mtaona.

Simba: Vipi mtani Kapumbu kafanyaje?

Yanga: Tulikuwa tunatest mitambo subiri siku Rivers United ya Nigeria, huwezi umiza wachezaji kwa bonanza.

Simba: Andaeni timu Rivers sio timu ya kitoto!

Yanga: Kocha wenu hana vyeti.

Simba: Jamaa jiandaeni huyu kocha ndio kawatafutia ninyi nafasi hiyo mnayocheza.

Yanga: Tunatoa kozi za Fifa Class A. Tunaye Profesa.

Simba: Mtani umerekebisha makosa ya mechi ya kwanza?!?!

Yanga: sisi tumekodisha Ndege ndio timu ya kwanza

Simba: Mtani, Rivers hao watakufunga tena jamaa washaweka ahadi ya goli 4

Yanga: Hatuongei sasa hivi majibu tarehe 19.

Simba: Haya ngoja tuonee....
 
Kelele zote hizo mwisho kwenye Mechi ya Ngao ya jamii.Tarehe 25/9/3/2021.Mwisho,mwisho,mwisho manake mtu mzima atakula kipigo watu wakavurugane.Muda utasema,Bado wiki moja tu mwisho wa tambo na majigambo pale mtu mzima mwenye makele kama mwanamke wa kizaramo atakapoliwa bila huruma
 
25/9/2021
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…