Utani Wenye Ukweli Kwa SIMBA: Huwezi kuchukua Gongo kutoka kwenye kopo la Maji-Poa ukaiweka kwenye chupa ya Bia halafu useme unakunywa bia

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Mashabiki wa simba na watu wote wapenda Mpira niwaambie tu hivi kua GONGO ni GONGO No Matter ipo kwenye Chupa gani.

Ujue Mashabiki wa Mpira Hasa Simba kwa hapa Tanzania wanaongoza kwa kushabikia Matokeo ila sio Mpira.
Niwaambie Ukweli ambao hamtataka kuukubali BENCHIKA Sio Kocha na hajabadili chochote kiuchezaji kwa SIMBA ila alichobadili ni Matokeo tu ya Currently.

So ukiwa Mtu wakushabikia Matokeo nasema ipo siku utajaaa kwa Mfumo na utapoteza.

Ndio hicho niliwahi waonya Pindi cha Pira OBJECTIVES Kua Mpira mliokua mnacheza ilikua ni swala la Mda kuja Kuaibika coz mlikua mnafurahia leo ila hamjui kesho itakuaje coz mlikua mnacheza Mpira Mbovu.

Na Saiv Baada ya kuja huyu BENCHIKA Mkajisahaulisha na Matokeo ya Wydad na Sare zile 2 ila hamkutaka kuangalia kua Mnaendelea Kucheza Mchezo wenu Uleule (MBAYA)

Na kwenye Football kesho ndio kitu cha Msingi sana na ndio Maana unaona Team Nyingi Dunian saiv zina sajili Makinda maana zinaitaka kesho Bora sio Hii Bora ya Leo.

Simba Mnajikita kwenye Furaha Ya Leo ila hamtaki kutengeneza Kesho yenu..

Ndio Maana Mtaona YANGA anapoteza Leo ila amecheza Mpira Mzuri Team kama hio inakuambia hivi... KESHO itakua Bora na Utafurahi,

Ndio Maana hata YANGA alipopoteza COMMUNITY SHIELD wengi walikua wanasema Tuna Team Maana waliona Team Inavyocheza so matokeo lilikua swala la Mda tu.

#Endeleeni.
#NyieBadoniGongoTu.
 
Imetandika vizuri ila natofautiana na wewe upande wa kocha. Kwangu Benchika ni kocha mzuri sana tu kama alivyokuwa Robert. Tatizo ni wachezaji hawafiti Kwenye mfumo. Kumbuka hata NABI alipofika Yanga kumalizia ule msimu timu ilikuwa tia maji tia maji. Makocha wa Kaskazini wanahitaji wachezaji wanaojituma sio mabishoo, Simba hawapo na waliopo umri umekwenda.
 
Naunga mkono hoja.
 
Mawazo yako mazuri sana mkuu
 
Ile community shield ndiyo nilianza kujua gamondi ameongeza kitu maana yanga alikuwa anachezea Mpira anavyotaka bila papara Huku timu nyingine zikitamani mechi iishe na papatu papatu zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…