Revodon
New Member
- Mar 8, 2013
- 1
- 0
Utapeli kwa njia ya mtandao umekuwa ukiongezeka kila kukicha kutokana na ukuaji wa tekinolojia ya utumaji na upokeaji pesa kwa njia ya mtandao, hususani simu. Tanzania ni mojawapo kati ya nchi za Afrika mashariki zinazotumia huduma hiyo, kwa mfano M-Pesa, Tigo pesa, Airtel money n.k.
Tigo pesa ndiyo huduma ambayo ningependa kuizungumzia kwani kama wakala wa huduma hiyo sijapata tatizo na mitandao mingine ya simu. Ilikuwa ni siku ya jumapili tarehe 23/03/2014 muda wa saa moja na dakika 47 za jioni ndipo alipokuja mteja dukani na kutoa pesa kwa njia ya Tigo pesa, nikapokea ujumbe mfupi wa Tigo pesa kwenye namba yangu ya uwakala iliyosomeka hivi,
Pesa imetoka ROGATI LASWAI kwenda JUMA SAID, 0719510180. Maelezo ni kama ifuatavyo: kiasi: Tsh 250,000. Mrejaa: Tsh 640. Kiasi taslimu: Tsh 250,000. Salio jipya: 1,353,272. Kumbukumbu No. C1140323.1946.P06582. Sasa unaweza kutuma Pesa kutoka akaunti yako ya CRDB kwenda akaunti yoyote ya Tigo Pesa.
Ujumbe huo ulimaanisha Juma Saidi alitoa Tsh 250,000 na hivyo nilipaswa kumpa hela taslimu. Kabla ya mteja kutoa pesa salio langu la Tigo Pesa lilikuwa Tsh 1,099,772, hivyo baada ya kupata huo ujumbe mfupi wa Tigo Pesa unaonyesha muamala kukamilika na salio langu kuongezeka sikuwa na shaka kabisa na kumpa pesa taslimu.
Ni baada ya mteja mwingine kuja kutoa pesa kwa njia ya Tigo Pesa ndipo nilipogundua kuwa mteja wangu wa awali hakuwa mteja bali ni tapeli kwani salio langu halikuwa limeongezeka licha ya ujumbe mfupi wa Tigo Pesa kuonyesha pesa kuongezeka. Nikachukua jukumu la kuwapigia simu customer care lakini sikupata msaada wa maana mbali na kuagizwa kufika kwenye ofisi zao na kitambulisho.
Nilienda kwenye ofisi za Tigo kuhusu tatizo langu lakini pia niliambulia patupu kwani hata Customer care niliyeongea nae alionyesha kutokuwa na msaada wowote, kwani baada ya kumwelezea alinijibu sasa sisi tutakusaidiaje kana kwamba hajui wajibu wake. Nikajaribu kupiga namba ya Juma Saidi kama ilivyokuwa kwenye ujumbe mfupi lakini haikuwa inapatikana, kwani imefungiwa. Ni dhahiri nlikuwa nimeshatapeliwa, hata kama ningekwenda polisi hakuna msaada wa maana ningeupata.
Swali ni kwamba aliyenitapeli alijuaje salio langu na kukadiria ongezeko ambalo lilikaribiana sawa na pesa ambayo ilitakiwa niwe nayo baada ya yeye kukamilisha muamala wake, kwani kulikuwa na tofauti kidogo ya Tsh 3500 tu. Hata hivyo, aliwezaje kuset simu yake hadi nikapata ujumbe ulionyesha dhahiri ni wa Tigo Pesa kwani sikuona namba yake ya simu bali ujumbe mfupi tu wa Tigo Pesa. Ni maswali ambayo bado kila nikijiuliza sipati majibu.
Naelewa fika kwa kutumia software mbalimbali za computer na simu hakuna kinachoshindikana. Utapeli huu ni tishio kubwa kwa huduma ya Tigo Pesa na jitihada za hali ya juu zinahitajika kukabiliana na aina hii ya utapeli. Inaelekea mawakala wengi watakuwa wametapeliwa bila kujijua kwani ni wizi unaondelea chini kwa chini, na kama una wateja wengi na hauna muda wa kuangalia salio mteja anapotoa pesa basi mwisho wa siku lazima utaangua kilio.