Utapeli hatari tigo pesa

Utapeli hatari tigo pesa

Revodon

New Member
Joined
Mar 8, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Utapeli kwa njia ya mtandao umekuwa ukiongezeka kila kukicha kutokana na ukuaji wa tekinolojia ya utumaji na upokeaji pesa kwa njia ya mtandao, hususani simu. Tanzania ni mojawapo kati ya nchi za Afrika mashariki zinazotumia huduma hiyo, kwa mfano M-Pesa, Tigo pesa, Airtel money n.k.

Tigo pesa ndiyo huduma ambayo ningependa kuizungumzia kwani kama wakala wa huduma hiyo sijapata tatizo na mitandao mingine ya simu. Ilikuwa ni siku ya jumapili tarehe 23/03/2014 muda wa saa moja na dakika 47 za jioni ndipo alipokuja mteja dukani na kutoa pesa kwa njia ya Tigo pesa, nikapokea ujumbe mfupi wa Tigo pesa kwenye namba yangu ya uwakala iliyosomeka hivi,

“Pesa imetoka ROGATI LASWAI kwenda JUMA SAID, 0719510180. Maelezo ni kama ifuatavyo: kiasi: Tsh 250,000. Mrejaa: Tsh 640. Kiasi taslimu: Tsh 250,000. Salio jipya: 1,353,272. Kumbukumbu No. C1140323.1946.P06582. Sasa unaweza kutuma Pesa kutoka akaunti yako ya CRDB kwenda akaunti yoyote ya Tigo Pesa”.

Ujumbe huo ulimaanisha Juma Saidi alitoa Tsh 250,000 na hivyo nilipaswa kumpa hela taslimu. Kabla ya mteja kutoa pesa salio langu la Tigo Pesa lilikuwa Tsh 1,099,772, hivyo baada ya kupata huo ujumbe mfupi wa Tigo Pesa unaonyesha muamala kukamilika na salio langu kuongezeka sikuwa na shaka kabisa na kumpa pesa taslimu.

Ni baada ya mteja mwingine kuja kutoa pesa kwa njia ya Tigo Pesa ndipo nilipogundua kuwa mteja wangu wa awali hakuwa mteja bali ni tapeli kwani salio langu halikuwa limeongezeka licha ya ujumbe mfupi wa Tigo Pesa kuonyesha pesa kuongezeka. Nikachukua jukumu la kuwapigia simu customer care lakini sikupata msaada wa maana mbali na kuagizwa kufika kwenye ofisi zao na kitambulisho.

Nilienda kwenye ofisi za Tigo kuhusu tatizo langu lakini pia niliambulia patupu kwani hata Customer care niliyeongea nae alionyesha kutokuwa na msaada wowote, kwani baada ya kumwelezea alinijibu “sasa sisi tutakusaidiaje” kana kwamba hajui wajibu wake. Nikajaribu kupiga namba ya Juma Saidi kama ilivyokuwa kwenye ujumbe mfupi lakini haikuwa inapatikana, kwani imefungiwa. Ni dhahiri nlikuwa nimeshatapeliwa, hata kama ningekwenda polisi hakuna msaada wa maana ningeupata.

Swali ni kwamba aliyenitapeli alijuaje salio langu na kukadiria ongezeko ambalo lilikaribiana sawa na pesa ambayo ilitakiwa niwe nayo baada ya yeye kukamilisha muamala wake, kwani kulikuwa na tofauti kidogo ya Tsh 3500 tu. Hata hivyo, aliwezaje ku’set’ simu yake hadi nikapata ujumbe ulionyesha dhahiri ni wa Tigo Pesa kwani sikuona namba yake ya simu bali ujumbe mfupi tu wa Tigo Pesa. Ni maswali ambayo bado kila nikijiuliza sipati majibu.

Naelewa fika kwa kutumia ‘software’ mbalimbali za ‘computer’ na simu hakuna kinachoshindikana. Utapeli huu ni tishio kubwa kwa huduma ya Tigo Pesa na jitihada za hali ya juu zinahitajika kukabiliana na aina hii ya utapeli. Inaelekea mawakala wengi watakuwa wametapeliwa bila kujijua kwani ni wizi unaondelea chini kwa chini, na kama una wateja wengi na hauna muda wa kuangalia salio mteja anapotoa pesa basi mwisho wa siku lazima utaangua kilio.
 
Pole sana na Hii ni case ya pili kuiona hapa JF ndani ya kipindi cha week tu, that means wanakuja juu sana
 
Pole sana Ndugu

Mie nasema hii ni issue ya baadhi ya Staffs wa Tigo Pesa.
Mitandao mingine ujinga huu hakuna.

Kama Kampuni ya Tigo haitafanya uchunguzi na kutimua Staffs wake wenye issue hizi kazi ipo.

Hizi issue ndio kama zile issue za Banks baadhi.
Kipindi cha nyuma utashangaa kwamba Mtu akienda kutoa pesa nyingi Bank mara kavamiwa njiani,kumbe pale Bank kuna mtu ndio issue zake kutonya nani anatoa kiasi cha pesa ili wamfuatilie wapige dili.
Na hao ndio wale wengine walikuwa wanatoa ramani ya jengo la Bank na majambazi kuvamia na kujua kila kitu kilipo kama vile wao ndio walikuwa wakandarasi wa hilo jengo.

Sasa ndio kama hawa watu wa TIGO,yaani kila siku lazima wakala mmoja aumie,na mbinu zote za kujilinda hata uwe mnjanja utaumia tu,maana watu wanasema angalia salio,sasa kama huyo hapo juu kachukua hatua zote lakini mwisho kaumia.

Mie nasema hii issue inafanywa na staffs wa Tigo,na mbaya zaidi nakumbuka waliteuwa Agents maalum kwenye ofisi zao ndio washughulike na line za Tigo pesa.Hapo napo ndio tatizo.
Mfano kwa hapa Zanzibar kuna watu maaluim wao ndio wanatoa lines hizo nakufanya usajili huo.na wamepewa ofisi humohumo Tigo kama wafanyakazi wa Tigo.

Panga pangua hapa jamaa wa ndani ya Kampuni wanahusika,na sijui kama sio hujma maalum hizi,na kama Kampuni ya Tigo haijaaangalia hili watapotea mapemaaaa.
Maana hata hiyo cutomer care yenyewe hovyo tu.
 
Pole sana ila usikate tamaa jaribu kufuatilia tena na tena
 
Mkuu uliyetapeliwa na wahanga wengine,
Kuna ujanja wa aina mbili hutumika.
Ujanja wa kwanza, tapeli hujitahidi kukuzoea na atasevu namba yake ya simu kwenye simu unayotumia kufanyia mwamala na namba yake ataisevu kwa jina la 'Tiggo pesa' au 'M-Pesa' kwa wa voda.
Kisha hutuma sms ya kuonyesha kuwa treansaction imefanyika. ingawa njia hii siku hizi imestukiwa sana.

Njia ya pili ni hii,
Tapeli hutumia simu ambayo ina huduma ya flash message.
Flash message huja moja kwa moja kwenye screen ya simu yako, huwa haiendi kwenye inbox, ingawa kuna baadhi ya simu huwa na option ya kuisev kwenye inbox lakini ni baada ya kuisoma kwenye screen.
sms hii inapokuja hainyoshi namba ya ilipotoka kwanza, huonyesha message moja kwa moja.

Tapeli anajuaje balance yako.
tapeli anaweza akaja kwa siku tatu mfululizo akaanza kukuuliza 'naweza kuweke/kutuma milioni mbili?, milioni moja, laki5 etc' jibu utakalompa litamsaidia yeye kukadiria balance yako.
njia nyingine tapeli huwasiliana na wahudumu wasiowaaminifu wa makampuni ya simu na kuangalia balance yako.

Nini cha kufanya.
Kuwa makini sana na mtu anayekuja mara kwa mara kuuliza kama anaweza kuweka/kutuma kiasi kadhaa.

kila unapofanya transaction, mbali na kupokea sms ya transaction lakini check your balance kala hujampa mteja pesa.
 
Mkuu uliyetapeliwa na wahanga wengine,
Kuna ujanja wa aina mbili hutumika.
Ujanja wa kwanza, tapeli hujitahidi kukuzoea na atasevu namba yake ya simu kwenye simu unayotumia kufanyia mwamala na namba yake ataisevu kwa jina la 'Tiggo pesa' au 'M-Pesa' kwa wa voda.
Kisha hutuma sms ya kuonyesha kuwa treansaction imefanyika. ingawa njia hii siku hizi imestukiwa sana.

Njia ya pili ni hii,
Tapeli hutumia simu ambayo ina huduma ya flash message.
Flash message huja moja kwa moja kwenye screen ya simu yako, huwa haiendi kwenye inbox, ingawa kuna baadhi ya simu huwa na option ya kuisev kwenye inbox lakini ni baada ya kuisoma kwenye screen.
sms hii inapokuja hainyoshi namba ya ilipotoka kwanza, huonyesha message moja kwa moja.

Tapeli anajuaje balance yako.
tapeli anaweza akaja kwa siku tatu mfululizo akaanza kukuuliza 'naweza kuweke/kutuma milioni mbili?, milioni moja, laki5 etc' jibu utakalompa litamsaidia yeye kukadiria balance yako.
njia nyingine tapeli huwasiliana na wahudumu wasiowaaminifu wa makampuni ya simu na kuangalia balance yako.

Nini cha kufanya.
Kuwa makini sana na mtu anayekuja mara kwa mara kuuliza kama anaweza kuweka/kutuma kiasi kadhaa.

kila unapofanya transaction, mbali na kupokea sms ya transaction lakini check your balance kala hujampa mteja pesa.

Thanks kaka mana umetoa ushaur mzuri sana
 
Yani ukiona ivo ujue kuna staff wa tigo ndo kashirikiana na uyo. Tapeli ktk kupata taarifa za account yako
 
Ninae mwizi wangu nimesha mkamata natafuta mwana sheria asimame nae kizimbani
 
Hizi huduma zinasaidia lakini muda mwingine zina maumivu, hasa hao tigo kila kukicha hapakosekani vijiusumbufu fulani fulani......hata sijui kwanini hawakui maana hata katika matumizi ya kawaida tu ya kupiga simu, unaweza kupiga simu zaidi ya mara nne unaambiwa unayempigia hapatikani, kama kuna watu wa tigo humu ndani pelekeni ujumbe kuwa mijadala kama hii kwenye mitandao sio mzuri kwa ustawi wa biashara yenu, jirekebisheni..........
poleni sana mkuu kwa huo utapeli uliokupata.
 
Ni kweli hii issue inafanywa na staff wa Tigo (Togopesa) system itakuwa inaonyesha balance ya kila agent so hiyo message inapikwa huko inapata baraka za kuongeza balance kisha wanadelete balance waliyoichota wezi hao. Tigo Pesa Management MPOOOOOOOOOOOO?
 
Buy chief baru
 

Attachments

  • IMG_284496210200859.jpeg
    IMG_284496210200859.jpeg
    34.1 KB · Views: 165
  • IMG_18141225320050.jpeg
    IMG_18141225320050.jpeg
    39.9 KB · Views: 153
  • IMG-20140225-WA0010.jpg
    IMG-20140225-WA0010.jpg
    40.9 KB · Views: 154
  • IMG_47255960797597.jpeg
    IMG_47255960797597.jpeg
    31.1 KB · Views: 161
Kaka mimi mwenyewe ni wakala wa tigo pesa ila nimeshatapeliwa na kwangu ni mteja salio lake linahamishwa usiku wa manane na sms inarudi kwake kuwa amehamishia kwa wakala sasa mteja anakuja asubuhi akidai hela yake ila hata yeye mwenyewe namuuliza ulitoa hela usiku anasema hakutoa sasa hela imehamishwaje? Na salio kwangu wakala halijaongezeka. Yaani nilienda hadi tigo makao makuu bila mafanikio hivyo hii kampuni ta tigo hasa upande wa tigo pesa ni matapeli haswaa mawakala tunaumia sana.
 
Back
Top Bottom