Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
-
- #61
Mbona unang'ang'ania sana wizi na utapeli wakati mimi nimetumia tu kama mfano wa kuwaeleza watu wenye akili nyingi licha ya kwamba hawajasoma sana.MTU anaibiwa kwa sababu kafika mjini kiss alifaulu chuo cha Udsm, IFM, DIT, Mzumbe, SUA, SAUTI, MAKUMIRA, n.k
Waliozaliwa mjini kuibiwa labda umkabe lakini sio maneno matupu, sijui kuibiwa kwenye Daladala, sijui Fiesta, sijui mtandaoni.
Mbona unang'ang'ania sana wizi na utapeli wakati mimi nimetumia tu kama mfano wa kuwaeleza watu wenye akili nyingi licha ya kwamba hawajasoma sana.
Sawa. Kwa heri. Safari njema.Mfano wako ndio kiini cha kutufanya tuelewe vizuri mada yako. Labda useme umekosea kutoa mfano.
Lakini huo wa wizi ni mfano mfu. Huwezi muibia mtu aliyesoma akaelimika.
Sawa. Kwa heri. Safari njema.
Kwa heri. Safari njema.Ndio hivyo, waliozaliwa mjini, born town, most wanted huwezi kuwafanyia huo upuuzi.
Naungana na wewe kuwa wapo waliosoma lakini bado ujinga upo vichwani mwao
Pole sanaShikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.
Ndugu zangu Watanzania;
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la (7) tu kwa sababu ya umasikini wa nyumbani kwao wakashindwa kuendelea na masomo.
Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sana hata ukikutana nao mtaani katika maisha ya kila siku, na kwa namna wanavyopangilia kazi zao au hata ratiba zao za kila siku, unajua kabisa huyu mwamba aliishia darasa la 7 kwa sababu ya umasikini tu na kama angesoma sana angekuwa mtu mmoja hatari kweli kweli.
Wewe jenga picha wale wezi wa pale kariakoo wanakuibia mfukoni bila hata wewe kujua kama kuna mkono umeingia ndani ya mfuko wako wa suruali na kuchukua pesa yako ya dagaa. Zile ni akili nyingi sana sema tu zimeelekezwa pahala pasipo stahili.
KISA KIDOGO CHA MIMI KUUZIWA KIPANDE CHA SABUNI KWA 20,000/= NIKIDHANIA NI SIMU
Nikiwa kidato cha 6 miaka hiyo ya 2000 na kitu, niliahi kuuziwa kipande kidogo cha sabuni nikidhani kuwa ni simu. Nilikuwa ninatoka Tabata Segerea nyumbani mama yangu mkubwa nilienda kumtembelea siku ya ijumaa jioni sasa nikawa ninarudi jumapili mchana ili nifanye maandalizi ya usafi wa nguo kwa ajili ya shule kesho yake ambayo ni Jumatatu.
Baada ya kushuka kutoka katika daladala pale mtaa wa Kongo akatokea jamaa mmoja rika langu akiwa ameshika simu aina ya nokia zile za jeneza za zamani akawa ananioneshea kwa ukaribu basi mimi nikaichukua ile simu nikaikagua vema kisha nikamuuliza bei gani, yeye akasema ni 20,000/=. Nikasema kimoyomoyo poa ngoja nichukue hii ngoma ili na mimi nikatambe huko mitaani.
Alafu hiyo pesa yenyewe sasa ndio nilikuwa nimepewa kama pocket money ya mwezi mzima na huyo mama yangu mkubwa. Yule jamaa rika langu kabisa akaniambia mwamba njoo huko hapo barabarani sana, basi mimi nikaenda, akanipa tena simu nikaikagua kwa mara ya pili, simu ipo sawa haina tatizo.
Sawa. Basi mwamba akaichukua simu akaiweka katika bahati fulani hivi ya kaki kisha na mimi nikampa pesa yake 20,000/= huyo nikaondoka. Kabla sijaenda mbali, baada ya kupanda daladala za kwenda home kwetu kurasini, nikaona ngoja nifungue bahasha nitoe simu yangu walau nicheze hata game la nyoka niji-keep busy, halooooo!
Nilikutana na kipande cha sabuni ya kodrai hahahahahaaaaa size ile ile kama simu ya Nokia ya jeneza (3310) kikiwa kinaniangalia tu. Kwa kweli roho iliniuma sana.
Ukizingatia 20,000/= ni pesa nyingi sana kwa miaka ile alafu mimi bado mwanafunzi sina majukumu mengi. Basi sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia hasira nilizokuwa nazo na nilipofika home nikafua nguo zangu kwa kutumia sabuni ya kipande ya 20,000/= hahahahaaaaa.
Kuna watu wenye akili nyingi lakini hawajasoma sana hususan huko vijijini. Unakuta mwanakijiji yeye hawajawahi kuwa na njaa bomani kwake. Miaka yote anavuna mahindi mengi, anafuga ng'ombe wake vizuri na anasomesha watoto kwa kuuza maziwa tu mpaka watoto wanamaliza form six. Siku akiamua kukuandikia barua, huo muandiko wake utadhani labda ni mwalimu wa secondary.
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi kweli. Je, ulishawahi kukutana nao (mbali ni wizi) katika maisha yako?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Alikutana na mkali zaidi yake...mi kuna dogo enzi za o level aliniazima kitabu chake...sasa baada ya kukitumia kama wiki nikakuta kitabu hakipo...ikapita kama siku tatu jamaa akaja akawa anataka kitabu chake...nikamwambia kuwa kitabu sikioni usikute kuna msela kanipiga..jamaa akasema basi itabidi ukakinunue ...nikamwambia mwanangu sina hela...akasema nipe ten, Basi bwana nkamlipa elfu kumi...baada ya kupita kama mwezi kuna dogo akaja akanitonya kuwa kile kitabu ulichoibiwa anacho yule dogo(Yule yule aliyeniazima)...mi nikauchuna, nikaenda dorm alilokuwa analala jamaa nikaangalia position aliyoweka tranka lake nikasepa..nikarudi dorm kwangu...siku tunafunga midterm ndo nikaona umefika wakati wa kumuumiza..siku tunamalizia pepa ya mwisho (Civics)..tuko kwenye pepa nikaomba ruhusa naenda toi...chap nikaenda dorm kwake nikabetua lock ya tranka lake nikapakia mazaga yake yote (Kikiwemo na kitabu nilichokilipia)nikaweka kwenye rasket, chap mpaka dorm kwangu uzuri tulikuwa nearby (Ye dorm 7 mi dorm 8) nikarudi class kumalizia pepa..nilivomaliza pepa chap nikabeba tranka langu nikasepa..nasikia mwana alilia kinoma..Mi kuna jamaa alitaka kuniuzia tecno W5 enzi hizo ndo zmetoka toka nafikiri dukan ilikua kwenye 180k+ jamaa akanifata akaniambia nimpe elf 40 aniachie dah nikamwambia nipe nikaikagua ni simu bad ipo kwenye Hali nzur Sana, nikambwambia chukua elf 35 akawa kama anakataa akaichukua akarudisha kwenye box wakati naondoka akaniita braza bas poa nipe hiyo huku ananipa simu kwenye box lake,
Nikamwabia leta nitest lain yangu kama itakaa hapo au ni ya kukata alivyonipa tu simu mkononi nikaiwasha alaf nikamlipa ile hela akaniambia leta nikuwekee kwenye box lake nikamwambia Sina shida na box, jamaa ilibid aniombe tu nimrudishie sim anipe hela yangu mi nikakataa nikamwambia tumeshakubaliana biashara imeisha, akataka kunivimbia akatoa wembe mfukoni mi nikachomoa kisu flan hiv nlikua natembea nacho, ye mwenyewe alisanda nikasepa kufika mbele nikadaka tororoo (bodaboda) nikaamsha zangu
Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi kweli. Je, ulishawahi kukutana nao (mbali ni wizi) katika maisha yako?Pole sana
Ukishamsoma mtu anaetaka kukufanyia uhuni we uspanic tulia tu ajilengeshe alaf unamfanyia uhuni mara 100 zaid yake maana ye akikubahatisha lazma ulieAlikutana na mkali zaidi yake...mi kuna dogo enzi za o level aliniazima kitabu chake...sasa baada ya kukitumia kama wiki nikakuta kitabu hakipo...ikapita kama siku tatu jamaa akaja akawa anataka kitabu chake...nikamwambia kuwa kitabu sikioni usikute kuna msela kanipiga..jamaa akasema basi itabidi ukakinunue ...nikamwambia mwanangu sina hela...akasema nipe ten, Basi bwana nkamlipa elfu kumi...baada ya kupita kama mwezi kuna dogo akaja akanitonya kuwa kile kitabu ulichoibiwa anacho yule dogo(Yule yule aliyeniazima)...mi nikauchuna, nikaenda dorm alilokuwa analala jamaa nikaangalia position aliyoweka tranka lake nikasepa..nikarudi dorm kwangu...siku tunafunga midterm ndo nikaona umefika wakati wa kumuumiza..siku tunamalizia pepa ya mwisho (Civics)..tuko kwenye pepa nikaomba ruhusa naenda toi...chap nikaenda dorm kwake nikabetua lock ya tranka lake nikapakia mazaga yake yote (Kikiwemo na kitabu nilichokilipia)nikaweka kwenye rasket, chap mpaka dorm kwangu uzuri tulikuwa nearby (Ye dorm 7 mi dorm 8) nikarudi class kumalizia pepa..nilivomaliza pepa chap nikabeba tranka langu nikasepa..nasikia mwana alilia kinoma..
Gangsters revenge...hamna kushtakiana wala kupelekana polisi...Ukishamsoma mtu anaetaka kukufanyia uhuni we uspanic tulia tu ajilengeshe alaf unamfanyia uhuni mara 100 zaid yake maana ye akikubahatisha lazma ulie
Ndio, nilishakutana nao.Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi kweli. Je, ulishawahi kukutana nao (mbali ni wizi) katika maisha yako?
Sawa mkuu.Ndio,nilishakutana nao.
Shukran, hata uwe smart vipi ipo siku hawa jamaa lazima watakutia mikononi, wezi bhana.Pole sana mkuu...
Ndio hivyo mkuu ingawa humu kuna jamaa mmoja anajigamba eti yeye ni mtoto wa mjini kitambo na hawezi kuibiwa.shukran,.hata uwe smart vipi ipo siku hawa jamaa lazima watakutia mikononi,wezi bhana.
Huwa nakutana nao ila nadhani ni mateja.. anakuonyesha simu nzuri halafu anakutajia bei chee.. huwa nawapita kama sijawaona vile..Je, ulishawahi kuwaona/kukutana na watu wana namna hii?