DOKEZO Utapeli mpya uliozuka mtandaoni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
UTAPELI MPYA ULIOZUKA MITANDAONI

Habari wana Jamii Forums

Kumekuwa na njia mpya ya utapeli mitandaoni ambayo inawaumiza wa Tanzania wengi na pia kuwaondolea uaminifu baadhi yao kwa jamii inayowazunguka. Utapeli umekuwa ukihusisha mtandao wakijamii wa Facebook kama daraja la kufanikisha hao matapeli kufanya kazi yao.

Kwanza matapeli hawa wamekuwa wakijimilikisha umiliki wa akaunti za watu za Facebook kisha kuzitumia katika kuwarubuni marafiki zake wa karibu kwamba kuna pesa zinapatikana kama Msaada kutoka UNICEF. Hivyo basi ukidanganyika na kuwafuata wanaenda kukumaliza.

Wamekuwa wakitumia namba za Safaricom katika kukamilisha nia yao ovu pengine ili wasiweze kujulikana kwa urahisi.

Ningependa wana jamii forum muwaamshe wa Tanzania juu ya utapeli huu

NB: Picha nilizo ambatanisha hapo chini nimfano wa sms za zinavyokuwa.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…