Viol
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 25,420
- 18,298
Habari za asubuhi wanajamvi,natumaini wote wazima kabisa na mnaendelea na shughuli zenu maofisini na nyumbani pia.
Napenda tu kuelezea kwa kifupi jinsi Scam/spams za internet zinavyoenea.Ila kutokana na hili jukwaa nizungumzie spams zinazohusiana na mapenzi,mara nyingi tunaweza kufanya dating online kwa kutumia sites mbalimbali,ila kuna wengine wanajiunga ili kutapeli wengine online,au unaweza kusema huyu mtu email zangu alizipataje au alipataje contacts zangu?Kuna software nyingi za kupata email za watu,mfano ''email extractor''hii software inatumika kutafuta email za watu kutokana na location unayoipenda,mfano ukisema utafute email za Tanzania unaweza ukapata emails za watu,sometimes ndani ya lisaa unaweza ukapata emails 500,1000 na kuendelea,kwa hiyo hawa watu wakizipata hizo email wanatumia software zingine kama ''Bulk email sender kutuma spams,na kwa wakati moja inaweza ikatuma spams hata 1000 kwa wakati mmoja.Jua ukitapeliwa huwezi kupata msaada mana internet wanayotumia IP ADDRESS zao wamezificha,Ambapo matokeo unapata emails kama hizi 'Dear, hope you are wonderfully well by The Grace, well, am joy, a nice
good looking girl, insearch of her true love with mutual understand, write
me back on (joy_babyand001@yahoo.com) to know me more.
''Greeting to you,
How are you and how is your work? i hope that all is well with you, My name is miss Debora,i know that you may be suprise how i get your email, dear i got your email today when i was browsing looking for honest partner at www.penpals.pl,then i feel to drop this few line to you , and i will like you to contact me through my email so that we can know each other and exchange our pictures, and we maybecome partner.
Remember the distance does not matter what matters is the love we share with each other.
i am waiting to hear from you soon.
regards Miss Debora
Nimewahi kuishi na watu kama hao na nimeona pia jinsi wanavyofanya kazi zao,wengi wao ni watu wa africa magharibi kama Nigeria,Ghana,Cameroon,Ivory coast n.k
Ukweli ni kwamba hata kama unatongozwa na msichana ujue unatongozwa na mwanaume na utakapoongea naye kwa simu au ukipiga simu anampa girlfriend wake uongee naye ili aweze kukulainisha.Pia pics wanazotuma ni pics fake kwa hiyo sio halali.
Silaha ya kwanza wanayotumia ni kujifanya wanahela na wanachotaka ni mapenzi ya kweli,anaweza akakueleza mali alizonazo mfano vyeo vya wazazi wake,jinsi walivyopata ajali na kuachiwa urithi,na n.k.
Hapo wao wanajikita kufanya romance na wewe online,kama ni mwanaume amekutongoza basi atakupa promise akupe ticket ya ndege umfuate au akuafuate na uishi naye pamoja,kufunga ndoa na mengine.Akishakuingiza kwenye romance anaweza anaweza kukutumia zawadi ndogo ndogo kama mikufu,pete,nguo kwa kutumia LDC ili mradi tu uamini,ukisha mwamini sana ndipo anaweza akakuambia anakutembelea
mara anakuambia amevamiwa na majambazi na walimlazimisha atoe kadi zake za benki na kutaja password(secret code) zake na hao majambazi wakajihamishia hela yake online kwa kutumia internet hapo hapo,kwa hiyo hana hela na anategemea kutumiwa hela mda wowote na ndugu zake.Kwa vile alishakuambia anakuja kukutembelea so atakuambia alishanunua ticket siku nyingi kwahiyo umsaidie hela kidogo kama dola 800,elfu 1000 kadri ya uwezo wako kwa mda anaposubiri kutumiwa hela na ndugu zake na wiki inayokuja atakupa hela yako face to face au atakutumia kwa njia ya western union,au account yako.Kwa vile ameshakuigiza kwenye hisia za mapenzi na ukamwamini,unaweza ukatuma hela umsaidie maana unajua kabisa ni mpenzi wako,ana biashara,gari,ndugu wenye hela.Akishapata hiyo hela anakata mawasiliano kwa vile anajua amefanikiwa kutoka kwao anaweza akaja tena kama mtu mwingine kwa style tofauti.Jua kwamba bank account yake ni account hewa ambayo iliyofunguliwa kwa kutumia Passpost aliyomwibia mtu kwa hiyo hakamatwi.Mwisho wake umetapeliwa na umeumizwa hisia za mapenzi.
Kumbuka unapojieleza mara ya mwanzo kwenye uhusiano wenu atapenda kujua kazi unayofanya ili ajue jinsi ya kukutapeli na kama akiona huna hela haendelei tena na wewe kuwasiliana.
Pia kuna njia nyingine ya kununua vitu online na ukatapeliwa hela na usipate ulichokinunua,kumbe ni bidhaa hewa ila hela imeenda kwenye account ya mtu,hiyo sintaeleza maana haihusiani na jukwaa hili.
Thanks kwa kusoma thread ndefu ingawa nimekuchosha kiasi flani.
By Excellent.