Utapeli unaofanywa na baadhi ya "maajenti" wasio waaminifu pale Magufuli Bus Terminal ukomeshwe!

Wabongo kukata tiketi mitandaoni wanaona ni usumbufu Bora atoke aende akatembee stand.
 
Vitambulisho na sare si matapeli wana forge vyao feki afu wanaendeleza utapeli kama kawaida. Hii nchi hata ukitaka mhuri wa Ikulu unapata ndo sembuse vitambulisho vya maagent wa stand ya bus!

Kutapeliwa ni uzembe/ujinga wa victim serikali haiwezi suluhisha hilo.
 
hii yote ni kutokana na tatizo la Ajira nchini kwetu vijana hawataki kufanya kazi ngumu
Malizia vijana hawataki kufanya kazi ngumu kwa malipo uchwara yaan unafanyishwa kazi ngumu alafu unalipwa malipo kiduchu unafanya kazi more than 12hrs alafu unalipwa afutatu yaan afutatu tu unafanyishwa kazi ngumu kwa zaidi ya masaa 12 alafu unalipwa afutatu na unapigishwa kazi ngumu za kuhatarisha hata Uhai wako na hapo hapo bado haujadharauliwa na kuonekana huna akili haufikiri nje ya box kwanini usiwataperi watu kwa siku ukaingiza more than 10 G's or even 20 G's?
 
Wa kulaumiwa ni watendaji wa serikali wenye dhamana ya kusimamia kituo hiko walipaswa waweke utaratibu mzima wa abiria na wasafirishaji wenye kulinda pande zote mbili
tena uwe wa wazi
 
Hiv watu mnapigwaje s mkatie tiketi officin au online au shekilango
 
Bora ya harali kuliko dhurma kaka
Dhurma hailipi kaka
 
Kuna dogo pale kitaa anafanya usalange Magufuli stand, kwa siku anakunja buku30 minimum na yeye sio agent wa bus lolote.
 
Nilipigwa hela na dada wa tumbo moja kabisa tangu hapo sijawahi kumuamini mtu yoyote linapokuja suala la hela. Inakuaje unatoa hela kulipia tiketi na basi haulioni tena sio ofisini? Majuzi nilikua nauza simu nikaongea na winga wa mjini akaniambia nimuachie simu ndani ya siku mbili atakua ashapata mteja nikasema thubutuuuuuu
 
Bora ya harali kuliko dhurma kaka
Dhurma hailipi kaka
Hujaumwa na njaa wewe yaan njaa haijakukaba alafu watu wanakuona km kiazi mdomo wa kuingiza watu King unao kwanini unashindwa kuutumia?
 
Bora ya harali kuliko dhurma kaka
Dhurma hailipi kaka
Kuongea ni rahisi sana mkuu sio ajabu unaandika comment yako ukiwa na goli linalokuingizia maokoto ya kuishi vizuri. Ufanye kazi masaa 12 unalipwa 4k toa nauli na kodi ya tumbo haubakiwi na chochote hivi unafanya mchezo
 
Kuongea ni rahisi sana mkuu sio ajabu unaandika comment yako ukiwa na goli linalokuingizia maokoto ya kuishi vizuri. Ufanye kazi masaa 12 unalipwa 4k toa nauli na kodi ya tumbo haubakiwi na chochote hivi unafanya mchezo
Kijijini si kuna mashamba kaka! Ukilima heka zako tano za mahindi ushakua millionaire. Hakuna aliyekushika shati kubaki mjini...
 
Ujinga tu, kwanini usikate kwenye basi moja kwa moja au ofisini?
 
Kijijini si kuna mashamba kaka! Ukilima heka zako tano za mahindi ushakua millionaire. Hakuna aliyekushika shati kubaki mjini...
Nenda kalime wewe au fungua kanisa ubiri matendo mema wengine waache wapambane kwa mbinu wanazoweza
 
Pia,siku hizi kampuni zinazojielewa hukatisha tiket online. Mimi huwa ninajilipua online tu. Nikifika stend sina taim na mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…