Utapeli wa ‘hiyo pesa tuma kwenye namba hii’ umeshika kasi, nimegundua mbinu ya kuwazuia, napendekeza haya yafanyike kuwakomesha

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Baada ya kugundua kila ninapojadiliana na mtu kwa simu a u meseji kuhusu masuala ya kutumiana pesa, ghafla natumiwa meseji za “hiyo pesa tuma kwenye namba hii”, napendekeza hili

TCRA watunge kanuni zifuatazo za kisheria

1.) Iwe ni sharti la kisheria kwa kila mteja anayetumiwa meseji za “hiyo pesa tuma kwenye namba hii” , au utapeli mwingine, kui-report namba hiyo kwenye namba maalum iliyowekwa na TCRA, na adhabu kali itolewe kwa wateja ambao watakaa kimya bila ku-report namba hiyo, ikiwemo faini na/ au vifungo jela.

Pia kanuni hii iwashurutishe mitandao ya simu kuitangaza kanuni hii mara moja kwa wiki kwa kutuma SMS kwa wateja wao juu ya kanuni hii mpya ya kisheria.

2.) Kwakuwa namba nyingi zinazotumika kufanya utapeli zilisajiliwa kimaghumashi kwa kuweka dole gumba na kisha kusajili namba nyingi bila mhusika kujua;

TCRA watunge kanuni ya kisheria ambapo mitandao ya simu italazimika kutuma meseji kwa namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA ambayo moja ya laini zake zimeripotiwa kutumika kwenye utapeli, hii inamaanisha kama mtu ana laini moja ya simu ambayo ndio anatumia yeye, ila kuna namba zingine zimesajiliwa kwa NIDA yake bila yeye kujua na zikaripotiwa kufanya utapeli, basi moja kwa moja mwenye NIDA yake atajua na atahitajika kufika polisi mara moja kutoa maelezo na kufuta usajili wa namba zingine baada ya kuonekana hausiki.

Hii ikifanyika kwa umakini na kwa muda mfupi, hawa matapeli wataishiwa namba za kufanyia utapeli, maana wahusika wenye namba zao watajulishwa papo hapo baada ya namba zao kutumika kufanyabu utapeli, na kabla hata hawajafanikiwa kutoa pesa waliyotumia, mwenye NIDA yake atakuwa amshazifuta laini za ziada kwa kutumia menu maalum ya SSD kwenye simu yake.

Nakaribisha maoni.

=========================
Kwakuwa inawezekana namba za marehemu pia zinatumika, mtu asipofika polisi ndani ya siku 2 au 3, namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA hiyo zinafungwa. Kama yupo hai basi ataenda kwa mtoa huduma wake kuuliza tatizo nini, na hapo ataelekezwa afike polisi

===========================
Pia italeta msukumo zaidi endapo kila atakaetumiwa meseji ya tuma pesa kwenye namba hii akaweka screensoot yake hapa.., walau tusijue haadi ya namba, na wenye majina yao wakiona wanaweza kufuatilia kama namba zao zinatumika vibaya


==========================
 
Jamani msitujadili sisi vibaka wa kawaida tunaomba na mafisadi kwenye sekta mbalimbali za serikali muwajadili na kutengeneza Sheria Kali ili wabanwe na vyombo vya dola.
Maana nchi hii mafisadi papa huwa hawaguswi ila sisi vibaka wa uswahilini kila siku mnajadili jinsi ya kutuangamiza!
 
Una hoja, usikilizwe,

Nyie vibaka wa elfu thelasini thelasini mnaandamwa huku majambazi ya mabilioni yakipigiwa salute huko wizarani.
 
Marehemu nao watahitajika kufika polisi!
Hilo la kutoa taarifa halijaanza leo, ni miaka na hakuna hatua zinazochukuliwa.
 
Hakuna jipya kwa maelezo yako halifanyiki
Mitandao yote ya simu ina ya kuripoti namba zote za utapeli ukiripoti tu wanaiblock
 
Mimi kama mtaalamu wa sheria, sidhani kama ni sahihi kutunga sheria/kununi nyingine za line za simu wakati sheria zilizopo bado hazijatekelezwa kikamilifu ili tuone changamoto zipo wapi.

Zaidi sana labda useme sheria zifanyiwe marekebisho iwapo katika utekelezaji wake (ambao bado) itaonekana kuna lacunae (gap).
 
Mbona wanaotukana viongozi wa serikali kwa meseji wananaswa hao vipi wengine? Ni uzembe tu wa TCRA kutowajibika.
Hawa wa ‘tuma namba hii’ wako wengi sana…, utahitaji resources nyingi sana kuwafuatilia wote, utafuatilia namba ipi utaacha ipi? Dawa ni huu mfumo ninaopendekeza, upo water tight, hachomoki mtu.
 
Marehemu nao watahitajika kufika polisi!
Hilo la kutoa taarifa halijaanza leo, ni miaka na hakuna hatua zinazochukuliwa.
Asipofika polisi ndani ya siku 2 au 3, namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA hiyo zinafungwa. Kama yupo hai basi ataenda kwa mtoa huduma wake kuuliza tatizo nini, na hapo ataelekezwa afike polisi.
 
Hakuna jipya kwa maelezo yako halifanyiki
Mitandao yote ya simu ina ya kuripoti namba zote za utapeli ukiripoti tu wanaiblock
Kwamba wanatuma meseji kwa namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA husika? Kwamba sasa ni kinyume cha sheria kutoripoti namba?
 
Hao matapeli wanalindwa na kulelewa na TCRA, polisi na pia makampuni ya mitandao husika. Kwa sababu wakiamua kuwadhibiti, ni zoezi la siku chache sana.
Daah, kwahiyo matapeli kumbe wapo humo humo ndani ya mfumo mitandao, TCRA na polisi, walio nje ya mfumo ndio hukamatwa sivyo?
 
Shida ipo wapi ukitumiwa meseji unafuta! Kwani unalizimishwa?

Tatizo lipo kwa watanzania wengi hatupo makini unatumaje pesa bila kuwasiliana na mhusika? Huo ni uzembe wa hali ya juu hasa kuhusu pesa?

Ushawahi kujiuliza hao matapeli wanatofauti gani na yale makampuni ya kubeti yanayotuma sms? Mbona yenyewe hayazungumziwi kama shida ni sms?

Kuna matapeli wakubwa na ni viongozi wa kuheshimika kwanini mamlaka zisichukue hatua?

Naomba kuhitimisha!

Watanzania wengi ni matapeli, wezi, na sio waaminifu iwe makazini au sehemu yoyote ile hata hao walio pewa jukumu la kusimamia sheria ndio hao hao wanazivunja.
 
Seen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…