FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Baada ya kugundua kila ninapojadiliana na mtu kwa simu a u meseji kuhusu masuala ya kutumiana pesa, ghafla natumiwa meseji za “hiyo pesa tuma kwenye namba hii”, napendekeza hili
TCRA watunge kanuni zifuatazo za kisheria
1.) Iwe ni sharti la kisheria kwa kila mteja anayetumiwa meseji za “hiyo pesa tuma kwenye namba hii” , au utapeli mwingine, kui-report namba hiyo kwenye namba maalum iliyowekwa na TCRA, na adhabu kali itolewe kwa wateja ambao watakaa kimya bila ku-report namba hiyo, ikiwemo faini na/ au vifungo jela.
Pia kanuni hii iwashurutishe mitandao ya simu kuitangaza kanuni hii mara moja kwa wiki kwa kutuma SMS kwa wateja wao juu ya kanuni hii mpya ya kisheria.
2.) Kwakuwa namba nyingi zinazotumika kufanya utapeli zilisajiliwa kimaghumashi kwa kuweka dole gumba na kisha kusajili namba nyingi bila mhusika kujua;
TCRA watunge kanuni ya kisheria ambapo mitandao ya simu italazimika kutuma meseji kwa namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA ambayo moja ya laini zake zimeripotiwa kutumika kwenye utapeli, hii inamaanisha kama mtu ana laini moja ya simu ambayo ndio anatumia yeye, ila kuna namba zingine zimesajiliwa kwa NIDA yake bila yeye kujua na zikaripotiwa kufanya utapeli, basi moja kwa moja mwenye NIDA yake atajua na atahitajika kufika polisi mara moja kutoa maelezo na kufuta usajili wa namba zingine baada ya kuonekana hausiki.
Hii ikifanyika kwa umakini na kwa muda mfupi, hawa matapeli wataishiwa namba za kufanyia utapeli, maana wahusika wenye namba zao watajulishwa papo hapo baada ya namba zao kutumika kufanyabu utapeli, na kabla hata hawajafanikiwa kutoa pesa waliyotumia, mwenye NIDA yake atakuwa amshazifuta laini za ziada kwa kutumia menu maalum ya SSD kwenye simu yake.
Nakaribisha maoni.
=========================
Kwakuwa inawezekana namba za marehemu pia zinatumika, mtu asipofika polisi ndani ya siku 2 au 3, namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA hiyo zinafungwa. Kama yupo hai basi ataenda kwa mtoa huduma wake kuuliza tatizo nini, na hapo ataelekezwa afike polisi
===========================
Pia italeta msukumo zaidi endapo kila atakaetumiwa meseji ya tuma pesa kwenye namba hii akaweka screensoot yake hapa.., walau tusijue haadi ya namba, na wenye majina yao wakiona wanaweza kufuatilia kama namba zao zinatumika vibaya
==========================