Utapeli wa kampuni ya tigo wakishirikiana na bima mkononi (milvik)

Hii huduma ya bima mkononi sasa hivi ni kama mbinu mpya ya mapato kwa mitandao hata vodacom wanayo na wekuwa wanapigia wateja wao simu mara kwa mara nami pia nikiwa mmoja wao lakini huwa nakataa maana hainiingii akilini nichange 55000/= kwa mwezi halafu upate changamoto upewe 40000/= kwa siku.
 
Hii katika bitu nasikitika ni kua licha ya serikali ya chama cha kijani kutokubali kutoa walipo, hawataki hata kutetea maslahi ya wananchi wao kwenye huduma zinazofanywa na third parties, yani ukisoma comment watu wengi wanasema hayo malalamiko juu ya hizo kampuni ni mengi ila serikali haizibani hizo kampuni mwisho wake wananchi tunakua watu wa kupigwa tu kila sekta
 
Hizi huduma za mtandaoni muwe nazo makini sana maana huduma za bima Kwa Tanzania hata hizi zenye ofisi ni issue nzito yaani wanakuja na mambo mengi mazuri mazuri huku hawakuelezi process za kufanya unapopata shida.

Sasa Kwa mtandaoni si ndio balaa maana ukienda Tigo watakuruka watamwambia hao wanaofanya hiyo kazi ni mbia na lazima atakuwa ame-click vigezo na masharti ambavyo mkija kuvisoma baadae mtakuta vinampa haki mtoa huduma.

hao ni washenzi sana tena mkeo alijikuta amejaa akakubali maana wakikupigia simu ukiwaandekeza wanaweza wakaongea hata dakika 20 alafu unawakatalia wanakomaa wachukue tu details zako hata kama hujiungi ili ukitafakari baadae ujiunge
 
Nimekosea hapo kidogo huwezi kuchanga 5500/=kwa mwezi halafu mtu akulipie 40000/= kwa siku.
Mimi mwenyewe ndo nimeshangaa, haiingii akilini eti ukatwe elf tano Mia tano (5,500/=) alaf ulipiwe upasuaji kweli?? Inamaana kabla ya kujiunga hata hamkufikiria hilo??

Yaani itakuhitaji uchangie miezi isiyopungua 8 ndo ipatikane hela wanayokulipia wao siku moja? Hata kengele ya hatari haikulia kichwani seriously??

Hii serikali mbona mnaipa kazi ya kuchakata mambo ambayo yangepambanuliwa na kichwa chako tu
 
Kuna uzi nilisoma inaonekana wanatumia mbinu ya delay technique maana unatumia kwanza ela yako then unapeleka vielelezo kama ulivyosema na ukipeleka vielelezo Kuna uwezekano unaambiwa vina mapungufu mara hakuna muhuri mara hivi hivyo ulete vielelezo vyenye muhuri na ukirudi hospital utaambiwa utaratobu wetu huo na hatufanyi Kwa matakwa mgonjwa yaani document wanaziverify Kwa kugonga muhuri pale wanapoandika madai ya kuomba kulipwa mfano NHIF etc. Kimsingi wamekosa uhalali wa kutoa bima maana bima inatakiwa ifidie gharama zako pasipo kuweka wewe chochote labda Kwa zile huduma ambazo bima haihusiki. Kwa maana nyingine hao jamaa huduma yao haitambuliki kwenye hospitali zetu na ndio maana hata ushirikiano unakuwa mdogo.

Kama Wana Nia njema walipaswa kuingiza makubaliano na hospitali ili ukienda tu unawaambia hospitali Kwa kutoa vielelezo vyako na hospitali inawasiliana nao.

Soma uzi huo chini, comment namba 6

 
Mamlaka inayosimamia bima ambayo ni TIRA ipo lakini haishughulikii hizi changamoto, hawa jamaa wanatakiwa kufutiwa usajili na kuburuzwa mahakamani kabisa!!
Unakuwa kama mgeni na hizi mamlaka,hapo watu washakula chao
 
Mantiki nzima ya bima unaielewa lakini?? Hebu tuambie bima yoyote uliyojiunga na namna unanufaika. Bima kiufupi ni mchange wengi wanufaike wachache kwa kile walichochanga wengi, ndiyo maana unaweza tibiwa Upasuaji wa milioni 5 kwa NHIF na michango yako ikawa chini ya milioni 1.
 
Hii dhulma inafahamika, ila kwa kuwa waTz ni wajinga, wanaendelea kujiunga
 
Tigo waliigawa huduma ya Bima kwa jamaa wa kampuni moja inaitwa Proin kama sikosei. Waliitoa huduma hiyo, kwa malengo ya kufanya iwe na ufanisi.
Na baadhi ya wamiliki wa kampuni hiyo ni jamaa ambao ni miongoni mwa waliofanikiwa kuchota zile hela za EPA ambao JK aliamuru warudishe ili wasishtakiwe.

Hawa Proin ndiyo wanatakiwa kutoa majibu.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…