Utapeli wa letshego (Faidika) Tanzania

Mlalamikaji daily

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2014
Posts
744
Reaction score
1,621
watajwa hapo juu Ni benki binafsi ambayo inakopesha watumishi wa Uma...

katika mikataba yao Kuna kipengele Cha kufuta mkopo endapo mteja ataamua kulipa Deni kwa mkupuo....


mwaka juzi nilikopa mkopo kwao Hawa jamaa ..

Sasa Deni limebaki Kama 2 m hivi pamoja na riba yao...

kwa bahati nikapata hela mwezi uliopita nikataka niwalipe ili waniachie salary yangu.... nikajaza fomu za kutuma viambata vyote nikaambiwa kusubiri siku 14,
baada ya wiki tatu Bado naambiwa eti niende makao makuu kufuatilia na Tena siwez kupata balance Hadi nisubiri ....

lengo lao nisifanikishe kuwalipa ili niendelee kukatwa tu wafaidike Kama jina lao...

tafadhali mnapokopa watumishi wa Uma kuweni makini...

muwe na jumatatu njema.
 
kwani ukilipa kwa mkupuo na kulipa kwa makato kila mwezi tofauti ipo wapi???
 
Asante kwa taarifa, wajanja tupo makini mno hatukopi huko tupo busy na bank kabisa kama CRDB na NMB
 
wee hudaiwi na hao wemejichanganya tuu, mwone mwanasheria wako mweleze hali ilivyo atakusaidia kisheria maana wee unavielelevyo vyote kuwa umemaliza deni mkuu
 
Mkuu siku ingine ujifunze

Nenda kakope benk zinazoeleweka wachana na huto tu-taasisi
 
vibenki hivi vya vichochoroni ni shida ukitaka kuwalipa utazungushwa wewe genda ubwele, sijui hawatakagi hela, nenda pale abc banc, byaport, na wenzao wa aina hiyo
 
Pole sana mkuu. Haya ndio matatizo ya watumishi wa umma.
 
vibenki hivi vya vichochoroni ni shida ukitaka kuwalipa utazungushwa wewe genda ubwele, sijui hawatakagi hela, nenda pale abc banc, byaport, na wenzao wa aina hiyo
Ni shida Sana lakini kupitia hizi social network tuelezane ukweli ili wengine wajifunze...
 
ukilipa kwa mkupuo tutapataje faida mkuu?.....
 
CRDB nao siku hizi ukitaka kulipa deni mpaka wakupe barua ufanye kazi ya ziada ni wasumbufu hasaa
Asante kwa taarifa, wajanja tupo makini mno hatukopi huko tupo busy na bank kabisa kama CRDB na NMB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…