Utapeli wa nyumba unaoshika kasi Mbagala Chamazi na Chanika

Utapeli wa nyumba unaoshika kasi Mbagala Chamazi na Chanika

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,647
Reaction score
9,604
Kuna wimbi la nyumba nzuri na za kisasa kwa mwonekano zinaziuzwa kwa bei chee 25m-45m Mbagala Chamazi na Chanika jijiji DSM.

Mchezo upo hivi:

Kuna jamaa wana viwanja vingi na wana mafundi wao ambao hujenga nyumba cha kiwango cha chini sana cement mfuko mmoja tofali 48+ tofali hufwatuliwa site na kujenga hapo hapo.

Bati gauge 32 wanapiga rangi wenyewe. Baadhi ya kuta wameweka play wood badala ya tofali kitaalam sana.

Kench zipo mbali mbali sana kubana matumizi ya mbao. Ndo maana nyumba zote laizma ziwe na gypsum kuficha mambo.
Nyumba huwa hazijakaliwa na watu means bado mpya.

Hazina lenta ndo maan lazima wapige plasta na kuweka gypsum kuficha. Kuna wataalam wa kuchanganya rangi ili kukubabaisha uingie kingi. Msingi tofali moja tu ishapanda

NB: Nyumba hizi hazichukui muda sana utaona nyufa balaa. Na walengwa wengi ni wastaafu ambao hutafuta nyumba za kuishi baada ya kustaafu.
 
Kama hii mkuu
tapatalk_1587313533061.jpg
 
Back
Top Bottom