Utapeli wa SBF - FTX lilikuwa jukwaa la kutakatisha fedha haramu na utapeli kuptia mgongo wa cryptos

Utapeli wa SBF - FTX lilikuwa jukwaa la kutakatisha fedha haramu na utapeli kuptia mgongo wa cryptos

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
1. Wakati FTX wanafanya fundraising, Sam Bankman Fried (SBF) alichukua yeye binafsi kiasi cha dollar za kimarekani milioni 300 kati ya 420.69 zilizokusanywa kutoka kwa wawekezaji.

2. Mwezi wa tatu mwaka huu, SBF alikutana na kufanya kikao cha siri na mwenyekiti wa Federal Reserve, Jerome Powell kwa saa 1. Walizungumza nini? Bado haijafahamika.

3. SBF na wakurugenzi wa FTX walichangia kiasi cha dola milion 70 kwa wanasiasa katika uchaguzi wa mdogo wa Marekani uliofanyoka wiki kadhaa zilizopita, na baada ya wiki chache wakatangaza kufirisika.

4. Jambo la kushangaza, wateja wa FTX ni asilimia 2 tu ndio walitoka Marekani, huku asilimia zaidi ya 22 wakitoka visiwa vya Cayman.

5. Timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors inakabiliwa na hatari ya kushitakiwa na kundi la watu waliopoteza pesa yao kwenye uwekezaji huo wa FTX kwa kuwa ilitumika kuitangaza FTX. Hii ni sawa na wana Kalynda kutaka kuishataki mitandao ya simu kwa kuwa iliruhusu wao kuweka na kutoa pesa Kalyanda. Funny.

6. Kampuni ya Alameda ambayo ni dada wa kampuni ya FTX iliwithdraw kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1.5 kati ya Oktoba 20 hadi november 2, na kiasi cha dola za kimarekani miliom 204 siku chache kabla kutangaza kufirisika kwa FTX. Hii inaonyesha kuwa hawa jamaa walijua mchezo wanaoucheza.

7. SEC ilitaka ichunguza FTX mwezi wa 3 lakini wajumbe wa 8 wa baraza la Congress walijaribh kuzuia kufanyika kwa uchunguzi huo. 5 kati ya wajumbe hao 8 inadaiwa walipokea michango ya kiasi cha dolar 2900 had 11000. Mchango ni jina zuri la kuficha neno rushwa.

8. FTX ilikuwa inamiliki asilimia 10 ya bank ndogo katika jiji la Washington. Benki hii ina wafanyakazi wa tatu huku asilimia hizo zilikuwa na thamani ya dola milion 11.5
Benki hii inajulikana kama Famington State Bank, ambayo kwa sasa imepewa jina jipya la Moondtone iko kwrnye mji mdogo wa Famingstone wenye wakazi 146 ina wafanyakazi 3 na tawi moja na ndio benki ya 26 kwa udogo Marekani.
FTX iliwekeza kwenye benki hii kupitia kampuni tanzu ya Alameda chini ya kampuni yake ya uwekezaji wa FBH hapo mwezi wa 3 mwaka 2022. Jambo la kushangaza iliwekeza dolar milion 11.5 kwa share asilimia 10 wakati benki ilikuwa ikishikilia kiasi cha dola za Kimarekani milion 10 tu za deposites za wateja. Yani eti FTX walithamanisha hiyo benki kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 115.
Yani ni kwamba, FTX waliithaminisha benki yenye assets zenye thamani ya dola za kimarekani milion 5.7 na pesa ya wateja dola milion 10 kuwa na thamani ya milion 115 dola.
Kwanink walifanya hivi? Inasemekana walitaka kuruka kikwazo kilichowahitaji kuwa na kibali cha kufanya shughuli za kibenki marekani jambo ambalo ni gumu kukipata.
Sasa inaaminika shughuli kubwa ya FTX ilikuwa ni kutakatisha frdha haramu wala sio crypto exchange.
 
Nilikuwa nawaambia hapa kwamba mkiwekeza kweny hizo kampuni wanakuwa na timing wanawazunguka nyuma kila mtu anachota chake.Then Wana wanajifanya wameundergo bankruptcy na kutumia majadili ya biashara kama Bloomberg kwamba wamefilisika kumbe wamepiga watu.

Hedge funds nyingi now zimekuwa ni scam kwa mgongo wa kufanya biashara za sarafu na forex, manager anatarget kiasi fulani cha pesa kikifika anatafuta sababu kwamba wamafilisika mara wameibiwa .

Watu wamawekeza sana washapigwa .kaeni kijanja!!
 
Back
Top Bottom