Kwa ujumla mimi sioni matatizo kwa haya makampuni. Haya makampuni mengi hayawaumizi wananchi. Serikali ndio inayowaumiza wananchi. Ksbb mpaka serikali kuifungia hiyo kampuni hakuna mwananchi alietoa malalamiko serikalini kuhusiana na hiyo kampuni.
Mfano hili sakata linaloendelea la LBL. Hakuna mwananchi alieenda serikalini kutoa malalamiko yoyote kuhusiana na LBL kwamba anadhurumiwa.
Bali serikali inasema imeifungia LB L ksbb haijajisajiri B.O.T.
Serikali ilitakiwa Ione wananchi waliowekeza kwa wingi kwenye hiyo LBL. Ilitakiwa ichunguze then kama swala ni usajiri wangeongea na LBL kwa taratibu ili waendelee kujisajiri. Negotiation hiyo inafanyika ili kuwanusuru wananchi waliowekeza humo. Sio kama hivi ghafla tu asubuhi unafungia kampuni ambayo unaona kabisa kuna watu wengi wataumia. Serikali ndio kila kitu kwa wananchi,basi ilitakiwa iwaone hawa waliojitupia humo ili wasalimike. Sio kama hivi shauri yao nani amewaambia wawekeze huko?