Utaratibu Gani Hutumika Kuoata Cheti Kwa Ndoa ya Kimila?

Utaratibu Gani Hutumika Kuoata Cheti Kwa Ndoa ya Kimila?

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Imekua kama desturi watu kukengeuka kutoka kwenye ndoa za kimila na kwenda za kidini yaani mtu anafunga ndoa kwa taratibu za kimila aghalabu kulipishwa mahari na itifaki nyinginezo na kisha anakwenda tena kufunga kanisani au msikitini

Kwa Kuwa zinapofungwa huko kwenye itikadi za dini kuna utaratibu wa kupata cheti cha ndoa, naomba kuuliza hizi zinazokamilika kwenye taratibu za kimila, utaratibu wake wa kupata cheti ukoje, nikianzia kuanzia kwenye tukio lenyewe ili liwe halali kisheria na kuweza kuwasaidia wanandoa kupata cheti, yaani nani anatakiwa kusimamia na ikiwa kuna waraka wowote unaotakiwa kutoka baada ya kuhitimisha kulipa mahari nk

Tushirikishane uzoefu na sheria zilizopo

asanteni
 
Nndoa za kimila hazina cheti, kama unataka cheti inabidi ufunge ndoa ya kiserikali kama si kidini.
 
Nndoa za kimila hazina cheti, kama unataka cheti inabidi ufunge ndoa ya kiserikali kama si kidini.
nimepitia inaonesha ili ukipate lazima utumia taratibu zilezile za ndoa nyingine, ikwemo kutangaza ndani ya siku 21 kabla ya ndoa na kushuhudiwa na Katibu Tarafa ambaye ndiye atahusika kukitoa cheti hicho
 
Back
Top Bottom