Utaratibu gani hutumika kurejesha mikopo HESLB?

Comfucious pedagogy

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
211
Reaction score
39
hivi ni baada ya mda gan mkopo niliokopeshwa naweza anza kukwatwa kwenye saraly?
 
Ni muda wowote kutegemeana na mwaajili wako(mkurugenzi) atakapo peleka taarifa zako, kama ni mwl kila halmashauri inautaratbu wate baadhi huwahi na nyngne huchelewa,kwani mimi nilikaa miezi 8 tu wakaanza kukata chao
 
Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha St. Augustine, mwaka 2012, nilipata 100% loan from HESLB. Nafanya kazi private sector, kuna bwana mmoja alikuja mwaka jana akidai anataka turejeshe pesa na yeye ni wakala wa bodi, tukamdai evidence akatupa vibali ambavyo vilipitwa mda wake.

Amerudi tena jana jumatano tar. 22/10/2014 na barua ina majina ya watu tunaofanya hapa na mimi ni mmoja wao nadaiwa kama 10M, penalty 1M, halafu sjui kitu gani 455,500/- Jumla kama 11.5M

Nina wasiwasi na huyu bwana kwasababu wengi niliomaliza nao wanadai hawajawahi sikia utaratibu huu wa mawakala, sasa isije kuwa ni kanjanja tuu tumpe hela zetu halafu tusimwone tena next time, pesa inatafutwa kwa taabu sana ndugu zangu.

Ieleweke kuwa nipo tayari kurejesha mkopo lakini katika utaratibu ulio sahihi.

Naomba msaada tafadhali kwa wale wenye ufahamu juu ya hili, haswaa majina ya mawakala wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
 
Never ever fall into that trap. Bodi wana utaratibu wao wa kurudisha mkopo kupitia kwa mwajiri moja kwa moja. Siku hizi wanakata 8%ya gross salary hakuna utaratibu wa mtu kukusanya madeni ya bodi. Huyo akija tena mpeleke polisi au kama mna namba yake mwambie aje kuchukua ela then toa taarifa polisi akamatwe ni mwizi.
 
Kweli kabisa ndugu yangu ila jamaa anataka tukatwe hiyo 8% inaingia kwenye akaunti ya bodi halafu anatoa risiti moja kwa watu wote! hata kama mpo kumi au ishirini sasa ishu ni kwamba je siku nikiondoka hapa nitakuwa vipi na evidence ya kuwa nilishatoa kiasi flani? Pia MAWAKALA NI AKINA NANII!!!!!
 
Ngoja nirudie tena. Kurejesha mkopo ni makubaliano kati ya mwajiri wako na HESLB na wala hawawezi kutuma mtu kiivyo. Be careful utaibiwa. Its simple akiwa polisi ukweli wote huwa utajulikana. Navyojua mie bodi wanamtumia mwajiri wako kukukata na anawasilisha kwao na huwa kiwango sahihi mwajiri anakijua pia baada ya kutaarifiwa na bodi. Asije mtu mtaani akakwambia ametumwa. Mjini hapa mtalia.
 
Kweli kaka nakuelewa sana sasa ndio nakomaa na mwajiri asiguse my acount manake ni majanga ntasababisha shida hapa jamaa anataka tukatwe kuanzia mwezi huu,. Kaja na barua flani anadai inatoka bodi yani sielewi kabisa
 

Inakuwaje kama nimeamua kujiajiri mwenyewe kwa ujasiriamali usio rasmi?
 
mie mpaka leo nimewakwepa hawa jamaaa,wala sidhani kama watanijua manaa hapa kwetu ni mwaka wannee wameanzankulamba mishaara ya watu,ila mm simo kwenye wadaiwaa
kwanza hela yenyewe walikuwa wananicheleweshea mpaka tuandamaneee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…