Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha St. Augustine, mwaka 2012, nilipata 100% loan from HESLB. Nafanya kazi private sector, kuna bwana mmoja alikuja mwaka jana akidai anataka turejeshe pesa na yeye ni wakala wa bodi, tukamdai evidence akatupa vibali ambavyo vilipitwa mda wake.
Amerudi tena jana jumatano tar. 22/10/2014 na barua ina majina ya watu tunaofanya hapa na mimi ni mmoja wao nadaiwa kama 10M, penalty 1M, halafu sjui kitu gani 455,500/- Jumla kama 11.5M
Nina wasiwasi na huyu bwana kwasababu wengi niliomaliza nao wanadai hawajawahi sikia utaratibu huu wa mawakala, sasa isije kuwa ni kanjanja tuu tumpe hela zetu halafu tusimwone tena next time, pesa inatafutwa kwa taabu sana ndugu zangu.
Ieleweke kuwa nipo tayari kurejesha mkopo lakini katika utaratibu ulio sahihi.
Naomba msaada tafadhali kwa wale wenye ufahamu juu ya hili, haswaa majina ya mawakala wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu.