GE2025 Utaratibu Mpya wa CCM kwa Ubunge 2025: Gharama, Mchujo, na Ukweli Usioambiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ashampoo burning

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2023
Posts
1,299
Reaction score
3,977
Utaratibu Mpya wa CCM kwa Ubunge 2025: Gharama, Mchujo, na Ukweli Usioambiwa

Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuja na utaratibu mpya unaowahusu wagombea wa nafasi ya ubunge – utaratibu ambao wengi wa watia nia hawakuujua mapema, na sasa unazidi kuzua taharuki na sintofahamu miongoni mwao.

Mfumo Mpya wa Mchujo

Tofauti na miaka ya nyuma ambapo mgombea akishinda kura za maoni za jimbo alijihakikishia tiketi ya ubunge, mwaka huu hali imebadilika. Huu hapa ndio mfumo mpya kwa muhtasari:

1. Watia nia wote wa ubunge huwasilisha majina yao kama kawaida katika ngazi ya jimbo.

2. Kamati ya Siasa ya Mkoa hupokea majina hayo yote na kuchagua majina matatu pekee... hapa majina yote ya watia nia yanaenda ccm mkoa kwanza kuchambuliwa

3. Majina hayo matatu yarudishwa jimboni, ambako wajumbe wa CCM jimbo watapiga kura kumchagua mmoja wanayemtaka...

4. Jina la mshindi linapelekwa Kamati Kuu ya CCM Taifa, ambayo ina mamlaka ya mwisho ya kupitisha au kukataa jina hilo.

5. Ikiwa Kamati Kuu haitaridhishwa na mshindi, inaweza kumpitisha mgombea mwingine kutoka wale waliokatwa awali, au hata kumleta mpya kabisa.

Athari kwa Watia Nia

Mfumo huu mpya unatoa picha ya wazi: kushinda kura za maoni si tiketi ya mwisho tena, na gharama ya kugombea ubunge kupitia CCM imeongezeka – si kwa pesa tu, bali kwa muda, nguvu, na mtandao wa kisiasa.

Wengi waliotia nia wamejikuta katika njia panda. Walidhani kuwa kuwashawishi wajumbe wa jimbo kunatosha, lakini sasa wanagundua kuwa lazima wawe na ushawishi katika ngazi ya mkoa na taifa pia.

Mchujo Wenye Siasa Nzito

Hii ni fursa kwa chama kupata wagombea bora, lakini pia kuna hofu: je, mfumo huu utatumika kwa haki au kisiasa? Je, nafasi ya wapambanaji wa kweli waliokubalika majimboni itaendelea kuheshimiwa, au itakuwa ni milango ya watu wachache wenye mamlaka juu?

Hitimisho

Kwa wagombea wa CCM 2025, ubunge sio tena ushindani wa jimboni pekee. Ni safari ya kisiasa inayohitaji maandalizi makubwa zaidi – kuanzia jimboni, mkoani hadi taifa. Wale wanaotia nia lazima wajipange si kwa maneno tu, bali kiuchumi, kiitikadi na kimtandao.

Na kwa wananchi, huu ni wakati wa kuhoji: Je, mfumo huu mpya unaleta haki na uwazi zaidi – au ni kikwazo kingine kwa demokrasia ya ndani ya chama?
 
Ni mtaji kwa Chama
Hizo hela za form ni nyingi mno
Ila hakuna la maana watakalolifanya wakiingia Bungeni.
 
Siingilii mambo yenu lakini naomba kuelimishwa ....

Ni kwa nini Samia na Nchimbi wamejipendekeza wenyewe na kujipitisha kuwa wagombea huku wakiweka masharti magumu kwa wagombea wengine ngazi za chini?. 🤔
 
Kwani walijipendekeza wenyewe? Mkutano mkuu ndio ulipendekeza na wakapitishwa
 
Je kuna muda na nafasi kwa yule aliyekatwa kwa kuonewa kuhamia CHAMA kingine?.
 
Sasa mtu ameshinda anakatwa na kuletwa ambaye hata hakuchukuwa fomu, huu si upendeleo na uonevu kwa upande mwingine?
 
Siingilii mambo yenu lakini naomba kuelimishwa ....

Ni kwa nini Samia na Nchimbi wamejipendekeza wenyewe na kujipitisha kuwa wagombea huku wakiweka masharti magumu kwa wagombea wengine ngazi za chini?. 🤔
Ajabu
 
Ni kheri wafanye kuwapitisha kama walivyomfanyia iddi amini dada ijulikane moja hakuna umuhimu wa kupigiana kura
 
Utaratibu Mpya wa CCM kwa Ubunge 2025: Gharama, Mchujo, na Ukweli Usioambiwa

Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuja na utaratibu mpya unaowahusu wagombea wa nafasi ya ubunge – utaratibu ambao wengi wa watia nia hawakuujua mapema, na sasa unazidi kuzua taharuki na sintofahamu miongoni mwao.

Mfumo Mpya wa Mchujo

Tofauti na miaka ya nyuma ambapo mgombea akishinda kura za maoni za jimbo alijihakikishia tiketi ya ubunge, mwaka huu hali imebadilika. Huu hapa ndio mfumo mpya kwa muhtasari:

1. Watia nia wote wa ubunge huwasilisha majina yao kama kawaida katika ngazi ya jimbo.

2. Kamati ya Siasa ya Mkoa hupokea majina hayo yote na kuchagua majina matatu pekee... hapa majina yote ya watia nia yanaenda ccm mkoa kwanza kuchambuliwa

3. Majina hayo matatu yarudishwa jimboni, ambako wajumbe wa CCM jimbo watapiga kura kumchagua mmoja wanayemtaka...

4. Jina la mshindi linapelekwa Kamati Kuu ya CCM Taifa, ambayo ina mamlaka ya mwisho ya kupitisha au kukataa jina hilo.

5. Ikiwa Kamati Kuu haitaridhishwa na mshindi, inaweza kumpitisha mgombea mwingine kutoka wale waliokatwa awali, au hata kumleta mpya kabisa.

Athari kwa Watia Nia

Mfumo huu mpya unatoa picha ya wazi: kushinda kura za maoni si tiketi ya mwisho tena, na gharama ya kugombea ubunge kupitia CCM imeongezeka – si kwa pesa tu, bali kwa muda, nguvu, na mtandao wa kisiasa.

Wengi waliotia nia wamejikuta katika njia panda. Walidhani kuwa kuwashawishi wajumbe wa jimbo kunatosha, lakini sasa wanagundua kuwa lazima wawe na ushawishi katika ngazi ya mkoa na taifa pia.

Mchujo Wenye Siasa Nzito

Hii ni fursa kwa chama kupata wagombea bora, lakini pia kuna hofu: je, mfumo huu utatumika kwa haki au kisiasa? Je, nafasi ya wapambanaji wa kweli waliokubalika majimboni itaendelea kuheshimiwa, au itakuwa ni milango ya watu wachache wenye mamlaka juu?

Hitimisho

Kwa wagombea wa CCM 2025, ubunge sio tena ushindani wa jimboni pekee. Ni safari ya kisiasa inayohitaji maandalizi makubwa zaidi – kuanzia jimboni, mkoani hadi taifa. Wale wanaotia nia lazima wajipange si kwa maneno tu, bali kiuchumi, kiitikadi na kimtandao.

Na kwa wananchi, huu ni wakati wa kuhoji: Je, mfumo huu mpya unaleta haki na uwazi zaidi – au ni kikwazo kingine kwa demokrasia ya ndani ya chama?
Kushinda kura za maoni haijawahi kuwa ndo umeteuliwa kuwa mgonbea wa chama kwa siasa za Tanzania. Hiyo ni kwa vyama vingi ikiwemo CCM na CHADEMA.
Kama ni mpya kwenye siasa ndo utashangaa
 
mfumo huu una mazuri mengi kuliko mabaya.kutokana na idadi ya wanasiasa kuwa wengi,lakini pia kufanana nguvu za kiushawishi kwa watia nia. unakuta jimbo moja lina waliochukua form 15 kati ya hao 15 ote wana elimu kubwa,wanaushawishi mkubwa,wana nguvu kipesa.basi hapa zisipotumika nguvu za aina hii watapatikana watu wa hovyo zaidi.
ndio maana ccm ni chama ambacho vyama vingi hapa africa vinajifunza kutoka kwao.
kosa la.ccm kubwa kwasasa ni kule kupoteza watu lakini kwenye mifumo wanajua kufikilia.
 
Athari kubwa ni kuongezeka kwa uchawa ngazi ya Taifa.
Hata kama mgombea anakubalika sana na Wajumbe na Wananchi bila kua chawa kwa viongozi wa chama Kitaifa hutoboi.
Ndio hali alisi, kujitoa ufaham kisa madaraka
 
Back
Top Bottom