GE2025 Utaratibu Mpya wa CCM kwa Ubunge 2025: Gharama, Mchujo, na Ukweli Usioambiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mbunge akiteuliwa na kupitishwa na Kamati kuu hatawajibika kwa wana jimbo, wakumbuke kuna wabunge husema wamechaguliwa na Mungu na huwa hawaipingi serikali kwalolote na hawaonekani majimboni
 
Mfumo ni mzuri ila wenye chujio ni wazuri, labda mchujo ungekuwa wa wazi siyo wengine wanakaa vikao usiku kupenyeza rushwa
 
uzuri mfumo.hauishii kwenye jimbo wala mkoa.kama mfumo unaangaliwa hadi taifa naamini watu wa usalama watawachambua vizuri zaidi.
tunaona wimbi limekua kubwa,hadi wachekeshaji kwasababu heti wana follower wengi huko.tiktok.wanajiona wanaweza kuwa wabunge. mala wanaanza kutuonesha wake zao walivyo na hips. sasa itakua serkali au selikali ya wachekeshaji.wengine wanajiita kabisa kua chawa kwamba uchawa unalipa. leo mpuuzi wa aina hiyo unampitisha awe mbunge....!!
 
Kwani walijipendekeza wenyewe? Mkutano mkuu ndio ulipendekeza na wakapitishwa
Acheni uzwazwa, haikuwa agenda ni walicheza nje ya box tu kuwa watu fulani liamsheni then tutaliunga mkono na fulani atasimama kulielezea vizuri na kisiasa litapita.
 
Hao Watatu wanaorudishwa Jimbo ni kupigiwa kura Watajinadi? Au Wajumbe wanapigia Kura jina bila kumuona na kumsikia mtia nia?
 
mengineyo nayo ni ajenda
Ajenda zinazopangwa kujadiliwa kwa umuhimu wake hupangwa kwa namba .... Ajenda ya kwanza, Ajenda ya pili n.k.

Iweje Ajenda muhimu kama ya kuteua na kutangaza wagombea kwenye uchaguzi mkuu iwekwe kwenye mengineyo tena kwenye mwaka wa uchaguzi? 😲
 
Aliyekwambia huu mfumo ni Mpya kakudanganya baada ya kujua wewe ni zuzu na utakuja JF mbio kuonesha uzuzu wako!
 
Aliyekwambia huu mfumo ni Mpya kakudanganya baada ya kujua wewe ni zuzu na utakuja JF mbio kuonesha uzuzu wako!
We na matacall kweli zamani mfumo ulikuwa mnapeleka majina yenu yote wajumbe wanapiga kura anapatikana mshindi jina linaenda kamati kuu taifa jina la mshindi.... mwaka huu majina yanaanzia kwenda kamati ya siasa ya mkoa ...kisha wanateua wao watu watatu tu..... pia KUMER LAKO
 
Kilichobadilika hapo ni hayo majina matatu ya kupeleka kwa wajumbe.

Vinginevyo kamati kuu siku zote imekuwa ikitoa maamuzi ya mwisho kwa washindi wa kura za maoni.

Labda kama ndio umeanza kufuatilia siasa.

Ugomvi mkubwa wa Magufuli na baadhi ya wana CCM ni ukataji waliofanya 2020, ilikuwa ni balaa na aijwahi kutokea washindi kukatwa vile.

Binafsi namkubali Magufuli kwa mambo mengi lakini alichofanya 2020 kwenye ukataji hakikuwa sawa kabisa.

Vinginevyo CCM imekuwa ikifanya hivyo miaka yote sema kamati kuu huko nyuma zilikuwa azikati watu sana unless wana makando-kando utakuta ni wawili watatu au hakuna kabisa.

Huko nyuma Irene Uwoya alishawahi shinda viti maalum akakatwa 2015, Bashe alimshinda Kigwangalla kabla Nzega aijagawanya 2010 akakatwa.

Sio jambo geni kamati kuu kuteua nje ya mshindi. Hayo majina matatu ndio geni lengo lao nadhani ni kupunguza zogo.
 
Huo utaratibu wa kurudiaha majina matatu mi naona ndio mzuri, kuliko kuwa na utitiri wa wagombea kiasi wajumbe mnachanganyikiwa halafu uchaguzi unachukua muda mrefu kwa wagombea kujinadi na makelele kibao. Na kamati kuu kuwa waamuzi wa mwisho ni sahihi kabisa sababu kuna mgombea anaweza kutokuwa na aifa akapita sababu ya pesa/rushwa.
 
Utaratibu wa kamati kuu kuwa mwamuzi wa mwisho huo ai mgeni
 
Watu wa usalama wanachambua wagombea wa CCM??
 
Serious kuna vyama vinaiga kinachofanywa na ccm? Duuu kazi ipo.
 
Kwa mtazamo wangu tunaenda kuokotewa wanaojua kusoma na kuandika tuu Tanzania ni ile ile na chama ndiyo kile tulichokijua,hivyo sharti kuwa chawa na uchawa uthibitike.Ni hayo tu,vinginevyo tutarajie miujiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…