pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 282
- 561
Salamu kwanza, kuna utaratibu mpya wa kuomba leseni za udereva ambao nitaelezea kama nilivyoelekezwa, unaingia katika tovuti ta TRA kisha unajisajili kwa kutumia nambari ya utambulisho wa mlipa kodi TIN unategeneza account kwenye portal yao (samahani kwa kuchanganya lugha maana hata bungeni walikosa tafsiri ya neno tax clearance) baada ya kutengeneza account uta-attach risiti yako ya EFD uliyolipia ada katika chuo ulichojifunzia na pia leseni yako ya kujifunzia almaarufu kama lena baada ya mwezi ambapo ndiyo wanaamini utakuwa umehitimu mafunzo utarudi tena kwenye account yako kisha utaambatanisha cheti cha kuhitimu na baada ya hapo utapangiwa tarehe ya test
Huu utaratibu ni mzuri kwa kuwa utasaidia kukusanya kodi ila changamoto zake ni kuwa mfumo mara nyingi unasumbua na pia idara ya elimu kwa mlipa kodi haijatoa elimu ya kutosha. Pia sina hakika iwapo "maboresho" haya yamelenga kukusanya kodi, kupunguza ajali au vyote kwa pamoja