abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
[h=2][/h]
Mamia ya abiria waliotarajiwa kusafiri jana kwenda visiwani Zanzibar, jana walikwama kuondoka kutokana na utaratibu mpya wa vitambulisho unaodaiwa kutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Nchini (Sumatra).
Kwa mujibu wa utaratibu, abiria haruhusiwi kukata tiketi ya kusafiri kwenda visiwani humo iwapo hatakuwa na kitambulisho, kikiwamo cha uraia.
Vitambulisho vingine ambavyo abiria anatakiwa kuwa na kimojawapo, ni pamoja na cha makazi, kupiga kura, kazi, leseni ya dereva, utambulisho kutoka serikalini au pasi ya kusafiria.
Baadhi ya abiria waliokwama kusafiri, walisema wamechelewa kupata taarifa hizo kwa kuwa hawaujasikia utaratibu huo katika chombo chochote cha habari.
Utaratibu huo ambao maelezo yake yamebandikwa kwenye kuta za ofisi za kukatia tiketi katika bandari za meli zinazokwenda visiwani humo, umeelezwa kuwa ulianza kutumika rasmi Agosti 13, mwaka huu.