Utaratibu na Watu wanaoruhusiwa kuwepo wakati wa kuhesabu Kura

Utaratibu na Watu wanaoruhusiwa kuwepo wakati wa kuhesabu Kura

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
IMG_20201026_081302_826.jpg

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Taifa Kifungu cha 72, kifungu kidogo cha kwanza kinaeleza kuwa:- Hakuna mtu yeyote zaidi ya wafuatao anatakiwa kuwepo wakati wa kuhesabu kura ,

a) Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi

b) Msaidizi wa msimamizi wa Kituo

c) Wakala wa Mgombea au mbadala wake

d) Mgombea

e) Afisa wa Polisi au mtu yeyote anayewajibika na suala la ulinzi kwenye mchakato huo

f) Msimamizi mkuu wa Uchaguzi, Msaidizi wa Msimamizi mkuu, au Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa

g) Mjumbe kutoka Tume ya Uchaguzi

h) Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa wa Uchaguzi kutoka kwenye Tume ya Uchaguzi, na

i) Mwangalizi aliyeidhinishwa kwa maandishi na Tume

Aidha Kifungu cha 73 kinaeleza kuwa:-Kabla ya Msimamzi wa Kituo na msaidizi wake kuendelea na zoezi la kuhesabu kura, mbele ya uwepo wa watu wote waliotajwa kwenye Kifungu cha 72 watafanya yafuatayo:-

a) Kuhakiki na kurekodi idadi ya watu wote waliopiga kura kwenye kituo husika

b) Kuhesabu na kurekodi idadi ya karatasi za kura ambazo hazijatumika, pamoja na kura zilizoharibika na kuziweka kwenye Bahasha maalum

c) Kukagua Muhuri au utepe ili kuhakikisha kuwa haujafunguliwa

d) Kufungua Muhuri au Utepe, na

e) Kufungua Sanduku la Kura
 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom