Utaratibu uendeshaji wa Uchaguzi Tanzania wadaiwa kudorora miaka ya karibuni

Utaratibu uendeshaji wa Uchaguzi Tanzania wadaiwa kudorora miaka ya karibuni

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Vyama Vikubwa vya Siasa nchini hasa vya upinzani vimekuwa vikilalamikia mchakato mzima wa uchaguzi kwenye nyanja zote, madai yao makubwa ni kuwa chama Tawala (CCM) kimekuwa kikibebwa na kupewa upendeleo wa wazi na mamlaka.

Vyama vingine vimekuwa vikinyimwa uhuru na haki sawa ya kuweza kufanya mikutano ya kisiasa kama ambavyo Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikifanya.

Pia vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamika kuwa kubanwa kwao tunatokana na wenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi na kufanya siasa kuwa wateule wa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Tawala. Hayati Magufuli enzi za Utawala wake aliwahi kuwatishia Wakurugenzi wa Halmashauri ambao kimsingi ndio wasimamizi wa Uchaguzi kuwa '' Awateue yeye, awalipe mshahara, awape magari na bado wamtamgaze mpinzani kushinda'' . Ukiangalia kauli hii ililenga kuwajengea hofu wasimamizi hao wa uchaguzi na wote tunajua kilichotokea uchaguzi mkuu wa 2020.

Kubanwa huko kumepelekea vuguvugu la vyama vya upinzani kudai katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ambavyo wanaamini kuwa utakuwa mwarobaini wa kufanya siasa safi kwa vyama vyote vya upinzania.

Leo Machi 21, 2022 Mwenyekiti wa Kikosi Kazi, Profesa Rwekaza Mukandara, amesema miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanasiasa juu ya uratibu na uendeshaji wa uchaguzi nchini Tanzania, ikiwemo kupungua kwa uhuru wa kufanya siasa nchini Tanzania.

Mambo mengine aliyoongelea ni kuhusu Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Akijibu kuhusu Tume Huru, Rais Samia amesema ''Tujiulize kwa hicho tunachokitaka kwamba Tume Huru, tujifunze kwa majirani zetu Je, pamoja na kuwa na hizo zinazoitwa Tume Huru hakuna migogoro? Hawatangazi matokeo na kukimbia Nchi? Maana halisi ya Tume huru ni nini hasa?
 
Back
Top Bottom