A
Anonymous
Guest
Nawasilisha kero yangu kuhusu utaratibu wa kuingia katika Kituo cha Mabasi Msamvu, Morogoro. Nilikuwa na safiri na tayari nilikuwa nimekata tiketi ya basi. Nilipofika getini na kuonesha tiketi yangu ili niingie ndani ya kituo, niliambiwa natakiwa kulipa tena shilingi 300 kama gharama ya kuingia kituoni.
Sijaelewa mantiki ya abiria ambaye tayari ana tiketi halali ya safari kutozwa fedha nyingine kwa ajili tu ya kuingia ndani ya kituo ili kulifikia basi lake. Naomba mamlaka husika itoe ufafanuzi kuhusu tozo hii, msingi wake na kwa nini haijumuishwi kwenye gharama za tiketi ya abiria.
Kilichonisikitisha zaidi ni namna nilivyohudumiwa. Nilipokubali kulipa shilingi 300 na kutoa noti ya shilingi 10,000, niliambiwa hakuna chenji. Hii ilikuwa majira ya saa moja jioni katika kituo kikubwa chenye abiria wengi kama Msamvu. Ilitokea mabishano yaliyosababisha nichelewe kuingia kituoni na nilikuwa karibu kuachwa na basi. Hatukusolve mpaka abiria mwingine alivyonilipia!