The unpaid Seller
JF-Expert Member
- Oct 27, 2019
- 2,113
- 6,251
Wasalaam,
Kwanza kabisa niwapongeze na kuwashukuru askari wetu wa jeshi la polisi kwa KUTEKELEZA MAJUKUMU yao, watu mengi huwabeza askari wetu lakini ukweli ni kwamba bila wao hata kaugali tusingeweza kulala kwa amani huku mitaani.
Jambo ninaloomba ufafanuzi ni kwamba ukoje utaratibu wa askari wetu kuvaa uniform wanapokuwa katika majukumu yao. Juzi nilikutana na jamaa wawili wamebeba bunduki AK 47 mtaani nilishtuka nikajua sekunde kadhaa mtaa utatekwa na ama majambazi wa kutumia silaha fasta nikaingia duka jirani kusikilizia milio ya risasi, cha kushangaza jamaa wakapita zao nikaja kugundua kumbe ni askari heee.
Sasa kwa mtindo huo si wahalifu wanaweza kutumia udhaifu huo wa kutovaa uniform wakatembea na mitutu na ghafla kuwa umbush watu!? Je siku hizi utaratibu wa askari kuvaa uniform ni option na sio lazima kama zamani?!
Kuna kituo kimoja cha polisi Mtibwa nilishawahi kwenda pale mwaka jana aise hakukua na askari hata mmoja aliyevalia uniform, hili nimekaaje wakuu.