Utaratibu wa kuapisha Wabunge waliochaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
1606741174693.png

Kwa mujibu Kanuni za Kudumu za Bunge Kifungu cha 30 (2) kinaeleza;

Endapo Mbunge atachaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu Spika atamuapisha katika:

b) Kikao chochote cha Bunge iwapo kuna Mkutano wa Bunge au;

b) Eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea

Baadaye Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata
 
Upvote 3
hata akipanga kuwaapisha uchocholoni au kutoka jalalani ni sawa tu kwa matakwa ya speaker
 
Ninaomba nakala ya hizi kanuni za Kudumu (2020) au link ya kuzipata
 
Unatumia kanuni wakati katiba ina provisions tofauti.

Lini katiba ilirekebishwa na kanuni ?
 
Na vipi kwa Mbunge aliyefukuzwa uanachama ktk chama chake cha Siasa?.
 
Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
Mpaka Chama husika kizitaarifu taasisi husika( Tume ya Uchaguzi na Bunge) kwa maandishi na sio kupitia vyombo vya habari ndio wabunge waliovuliwa uanachama watakoma kuwa wabunge

Kuna ushahidi kupitia vyombo vya habari kwamba wabunge 19 wa viti maalumu wa CHADEMA wamevuliwa uanachama na chama chao. Hakuna ushahidi hata wa kauli tu ya kwenye vyombo vya habari kwamba CHADEMA wameshaiandikia NEC barua kuitaarifu maazimio yao ya kuwavua uanachama hao wabunge wao.
 
Umejuaje?.

Kama ushahidi uliopo kupitia vyombo vya habari kuwa wanachama 19 wa CHADEMA ambao ni wabunge wamevuliwa uanachama, unaonekana sio njia rasmi huo ushahidi wa kauli kwa vyombo vya habari kutaarifu kuwa wameandika barua kwa NEC na Bunge utasaidia nini? Ama ndio itakauwa rasmi kama ulivyoeleza awali?
 
Hoja yangu ni kwamba CHADEMA haijasema hadharani kama wamewaandikia NEC kuwataarifu rasmi uamuzi wa Kamati Kuu yao wa kuwavua uanachama hao wabunge. Kauli aliyoitoa Mbowe ni kwamba milango ya kuomba radhi iko wazi na hiyo inaashiria barua kwa tume haitakwenda karibuni
 
Hivi kwann wabunge wa kuteuliwa had sa hv hawajaapishwa mbona wa viti maalum ilikuwa mapema tu,hoka c kuwaapisha haraka wawahi kuwatumikia wananch au??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom