Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ni aina fulani ya kukosa maarifa, upotezaji muda au ujuha kuamka kila siku asubuhi kufagia uani kwako, mbele ya nyumba yako au katika biashara yako kama hakuna pavement blocks, sakafu ya zege,/cement, tiles au lami. Unakuta mtu anatimua vumbi mtaa mzima kwa minajili kwamba anafagia kufanya usafi! Huo ni uchafuzi wa mazingira na sio usafi.
Nakumbuka hata tukiwa shule ya msingi na sekondari tulikuwa tunagaiwa maeneo ya kufanya usafi lakini kikubwa kilichokuwa kinafanyika ni utimuaji vumbi tu kila siku asubuhi halafu tunaingia darasani tumepauka kama vumbi lenyewe. Sehemu yenye vumbi, udongo au mchanga inakuwa na mashiko zaidi kuokota takataka kwa mikono ikiwa mmeshindwa kudhibiti utupaji wa holela wa takataka kwa kuweka dustbins.