Mropoka Hovyo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2023
- 446
- 1,253
Kila kitu kimekwisha wakuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye jina nenda mahakamani wakupe hati ya kiapo ya kumtambuwa marehemu kwa majina yote kwamba ni majina yake.Wakuu naomba kujua utaratibu umekaa vipi? yani napaswa niwe na vitu gani vya muhimu zaidi Ili mchako uweze kwenda kwa haraka.
Mpaka sasa na muhtasari wa kikao na Kibali cha Mazishi tu na hichi Kibali cha Mazishi nacho jina lililotumiaka la baba mzazi si lile ambalo marehemu alilokuwa analitumia kazini, Kwahiyo nalo naomba kujua nalisolve vipi hili nalo.
Pia naomba kujua barua nayoenda kuchukua kwa mwenyekiti wa mtaa ni ya kunitambulisha kama msimamizi wa Mirathi au ya nini hasa.
Dr Matola PhD OKW BOBAN SUNZU msaada wenu pls na wengine mnaojua haya mambo.
Hapo mkuu kuna mambo ya msingi utatakiwa kujiandaa kukabiliana nayo mahakamani. Unatakiwa kuthibitisha kwa nini wewe ni mnufaika pekee.Marehemu ni kaka yangu.
Bado hujanishawishi, i smell rat.Hizi pesa hazina mgawanyo wote ule kiufupi mnufaika ni mimi peke yangu wakuu.
Usahihi ni kwamba pesa za marehemu zilizopo bank account inafungwa zinalipwa kwenye account ya mahakama, wanufaika wanajaza fomu na mgawanyo wa pesa hizo na account number mahakama ndio inawaingizia pesa wanufaika kwenye account zao.Hapo mkuu kuna mambo ya msingi utatakiwa kujiandaa kukabiliana nayo mahakamani. Unatakiwa kuthibitisha kwa nini wewe ni mnufaika pekee.
Wanufaika wa mirathi ya mwanaume mume ni mke, watoto na wazazi. Ikiwa mke hayupo, ni watoto na wazazi, ikiwa watoto hawapo ni wazazi na ndugu.
Mahakama humpa kipaumbele mke halali wa marehemu kuwa msimamizi wa mirathi, otherwise kuwe na sababu za msingi za kutopendekezwa na kikao cha ndugu. Hata wakati wa kusikiliza shauri utasisitizwa watu muhimu kama hao wasikose,mke, wazazi na watoto. Itaenda hivyo kwa Msajili wa Vizazi na Vifo mpaka Benki watachukua tahadhali hiyo kwamba kwa nini ni wewe na sio mke au watoto.
Ukifanikiwa kuithinishwa na mahakama utapewa fomu na. 6 kujaza mgawanyo wa hiyo fedha ya benki. Itaandikwa barua kwenda kwa meneja wa benki kupitia mahakama ya wilaya ikiielekeza kufanya malipo. Kama mirathi haina changamoto italipwa moja kwa moja kwa wanufaika, tofauti na hapo itakipwa mahakama ili igawe yenyewe.
Kwa hivyo mahakama inapoona mnufaika ni ndugu na sio mke, watoto na wazazi, huchukua tahadhali kubwa sana wasije kukupitisha kisha kesho akaja mtu kuweka pingamizi. Ndio maana husikia kesi za mirathi zinaweza kwenda hata miaka 10.
Wakuu watanisahihisha kama kuna sehemu nimechanganya
Inachukua muda gani mahakama ikishapokea pesa kama Kila kitu kimekamilika kulipa wahusika,inachukua muda gani?Usahihi ni kwamba pesa za marehemu zilizopo bank account inafungwa zinalipwa kwenye account ya mahakama, wanufaika wanajaza fomu na mgawanyo wa pesa hizo na account number mahakama ndio inawaingizia pesa wanufaika kwenye account zao.
Kama hakuna tatizo ni mapema iwezekanavyo. Fuatilia kwa mhasibu wa mahakama kujua kama kuna shida, kama yeye ameshalipa basi issue itakuwa hazina ndogo huwa wana urasimu usipokuwa msumbufu. Wanaweza kuona tatizo wakakaa kimya bila kusema, kwa hiyo usiache kuwasumbuaWakuu OKW BOBAN SUNZU na Dr Matola PhD huwa inachukua mda gani mahakama kuwalipa wanufaika baada ya kumalizika taratibu zote. Nauliza hivyo kwasababu tunasubiria tangu tarehe 22 mwezi uliopita pesa ziingizwe kwenye akunti ya mama ambaye ni mnufaika lakini mpaka sasa ni hakuna kitu.
NB; Pesa zilishahmishiwa kwenye akunti ya mahakama tangu tarehe 20 mwezi 9.
Ulisema wewe ni ndugu wa marehemu na kwamba ni mnufaika peke yako🤔something’s fishy here! Now unaulizia pesa zima chukua muda gani kuingia kwenye akaunti ya ‘Mama’ ambaye kwa maneno yako naye ni “mnufaika”.Wakuu OKW BOBAN SUNZU na Dr Matola PhD huwa inachukua mda gani mahakama kuwalipa wanufaika baada ya kumalizika taratibu zote. Nauliza hivyo kwasababu tunasubiria tangu tarehe 22 mwezi uliopita pesa ziingizwe kwenye akunti ya mama ambaye ni mnufaika lakini mpaka sasa ni hakuna kitu.
NB; Pesa zilishahmishiwa kwenye akunti ya mahakama tangu tarehe 20 mwezi 9.
Mambo ya mahakama yapo taratibu, sisi tunasubiri huu mwezi wa 4Wakuu OKW BOBAN SUNZU na Dr Matola PhD huwa inachukua mda gani mahakama kuwalipa wanufaika baada ya kumalizika taratibu zote. Nauliza hivyo kwasababu tunasubiria tangu tarehe 22 mwezi uliopita pesa ziingizwe kwenye akunti ya mama ambaye ni mnufaika lakini mpaka sasa ni hakuna kitu.
NB; Pesa zilishahmishiwa kwenye akunti ya mahakama tangu tarehe 20 mwezi 9.