Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,355
- 14,408
Wakuu habari za siku nyingi?
Bila kupoteza muda ni kwamba tunaishukuru Serikali yetu kwa kutusaidia kupata soko la mahindi lakini tunalia na NFRA.Siku ya jumanne iliyopita,tarehe 24/07/2024; Nilipeleka mahindi yangu NFRA kituo cha Kakozi,mkoa wa Songwe.
Nikaelekezwa kuwa niyachekeche nikafanya hivyo.Nikaomba mifuko kwaajili ya ku rebag nikaambiwa imeisha nikaja kupata Jumatatu ya wiki hii ikawa haitoshi,nikaambiwa ni rebag hivyo hivyo wataniongezea.
Tokea hiyo jumatatu mifuko hawataki kunipa wanasema hadi nipime mahindi ambayo nime rebag,nikiwaambia wapime hawataki wanasema wako bize; Nawaambia sasa kama kunipa mifuko hamtaki na kupima pia hamtaki sasa mnataka nini?
Leo hii wamekuja kupima mzigo wa jirani yangu nilipowaomba waje wanipimie wamegoma eti wako bize.Kumbuka nalala lodge natumia gharama za chakula.
Aidha ukiacha usumbufu huo pia kuna vigharama vingi sana, kuna kuwalipa walinzi, kuchekecha mahindi ni gharama zako, ku rebag, kushona mifuko na kuipeleka kwenye streka, zote ni gharama zako.Mimi ni mara yangu ya kwanza mahindi.
Serikalini, aisee kwa hali niiliyoiona ni dhahiri bora uuzie tu Walanguzi hata kama bei zao ni ndogo, inauma sana. Ajabu ni kwamba waliokuja kwa kuchelewa wanahudumiwa fasta na kukuacha wewe uliyetangulia kufika.
OMBI LANGU KWA SERIKALI
1. Ninamuomba Waziri wa Kilimo aingilie kati hali hii,asione watu wanatorosha mazao nje ya nchi. Wakulima tunateseka kila kona kuanzia shambani hadi kwenye kuuza mazao uliyolima kwa jasho.
2. Aidha naomba Wizara ya Kilimo ingeteneza mfumo mzuri ambapo Wakulima wakifika kuuza mazao NFRA wawe wanasaini kwa dole gumbu kwenye mtandao ambapo taarifa zake zitaonekana hadi Makao makuu na akikaa muda mrefu hajahudumiwa basi wahusika waulizwe kwanini mkulima huyo amekaa muda mrefu hivyo?.
Ni hayo tu