KERO Utaratibu wa kukusanya fedha za kuzolea takataka huku Mbagala Kilungule haueleweki na unakera

KERO Utaratibu wa kukusanya fedha za kuzolea takataka huku Mbagala Kilungule haueleweki na unakera

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Katika eneo la Mbagala Kilungule, kuna changamoto kuhusu utaratibu wa ukusanyaji wa fedha za taka. Wananchi wanalalamikia kufikiwa na wakusanyaji wa ada hizo mara tatu au zaidi, huku wakipewa risiti zenye taarifa tofauti.

Wananchi wanapouliza kuhusu hali hiyo hawapati majibu ya kueleweka, na wakati mwingine hawapati majibu kabisa. Jambo hili linazua maswali, hasa ikizingatiwa kuwa gari la taka hupita eneo hilo takribani mara moja kwa mwezi pekee.

Tunaiomba mamlaka husika kufuatilia suala hili kwa kina, kuweka utaratibu unaoeleweka wa ukusanyaji wa ada za taka na kuhakikisha fedha hizo zinafika katika matumizi yaliyokusudiwa.
 
Back
Top Bottom