Utaratibu wa kununua kiwanja/ardhi

Utaratibu wa kununua kiwanja/ardhi

mkweli wa mambo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2013
Posts
329
Reaction score
180
Habari ndugu, jamaa na marafiki wote humu.

Leo nimeona niwe mkweli na muwazi ili kuepusha matatizo ntakayoyapata kama nisipouliza hili jambo. Kiukweli mimi jamani sijawahi kununua kiwanja (ardhi) katika maisha yangu, nashukuru mungu amenijalia kidogo naweza nkatimiza azma yangu ya kununua kiwanja mwezi ujao.

Sasa wadau kutokana na utapeli uliokithiri pamoja na matatizo mengi niliyokuwa nikiyaona kwa wenzangu na ndugu zangu wanaponunuaga viwanja yananipa wasiwasi wa kufanya jambo hili bila kuuliza

1. hivi ni vitu gani hasa vya kuzingatia kabla ya kununua kiwanja ili kuepuka utapeli?

2. je kuna utaratibu maalumu wa kisheria katika mchakato mzima wa kuuza/kununua kiwanja?

3. Nikishanunua kiwanja, je ni document zipi natakiwa kuwa nazo kama kiashilio halali kuwa mimi ndio mmilika halali wa kiwanja hicho.( nasikia kuwa unapewa hati ila ndoivo tena mwenzenu hata sample ya hati siijui,so hata nikipewa hati ya uwongo mi ntakubali tu, naombeni kama kuna mwenye sample ya hati halali mkinionesha ntashukuru sana)

4.je ,biashara hii ya kuuziana kiwanja inafanywa na watu wangapi? Ni mimi mnunuaji na muuzaji tu au kuna watu wengine pia wanatakiwa wawepo?

Nitangulize shukrani zangu kwa wadau naamini JF ndo sehemu pekee ya kupata mwongozo ulio sahihi.

Kabla cjaanza kukushauri kwanza upo mkoa gani??
 
Kama kiwanja kimepimwa basi utapewa hati inayotolewa na ardhi

Kama hakijapimwa basi kuna hati za kijiji/ karatasi za mauziano

Siku ya kununua unatakiwa uwe na mashahidi pia vyema mauziano yenu mkafanyie serikali za mtaa ingawa wanakata 10%
Na mjumbe wa mtaa awepo
 
asante sana kwa kunifahamisha mkuu
 
Kama kiwanja kimepimwa basi utapewa hati inayotolewa na ardhi

Kama hakijapimwa basi kuna hati za kijiji/ karatasi za mauziano

Siku ya kununua unatakiwa uwe na mashahidi pia vyema mauziano yenu mkafanyie serikali za mtaa ingawa wanakata 10%
Na mjumbe wa mtaa awepo

Mkuu hiyo ya 10% ilishaondolewa katika utaratibu,haipo tena na si lazima.Ila tu aandae hela ya kumpoza mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
 
Mkuu hiyo ya 10% ilishaondolewa katika utaratibu,haipo tena na si lazima.Ila tu aandae hela ya kumpoza mwenyekiti wa serikali ya mtaa.

mkuu unaweza kunisaidia hili tamko ili niende nalo?maana kuna sehemu nimechukua kiwanja naona jamaa wananitaka nilipe 10%
 
ni vema umekuwa mkweli mapema kuliko kuingia chaka, cha kwanza ni kujua kama kiwanja kimepimwa au la?
kama kimepimwa na kina offer basi mchakato mzima unaanzia Manispaa husika ya kiwanja kilipo pale utaenda ofisi za ardhi. na kama hakijapimwa basi nenda serikali za mtaa kuangalia kama eneo haliko katika barabara ama huduma za kijamii na ukiisha jiridhisha basi nenda kwa mwanasheria asimamie mauziano hayo.
 
Kama kiwanja kimepimwa basi utapewa hati inayotolewa na ardhi

Kama hakijapimwa basi kuna hati za kijiji/ karatasi za mauziano

Siku ya kununua unatakiwa uwe na mashahidi pia vyema mauziano yenu mkafanyie serikali za mtaa ingawa wanakata 10%
Na mjumbe wa mtaa awepo

Kwa sheria ipi inayosema mjumbe wa serikali za mtaa awepo?
 
Back
Top Bottom