Utaratibu wa kuombea maji au mafuta kisha ukawapa watu watumie upo katika dini zote.

Utaratibu wa kuombea maji au mafuta kisha ukawapa watu watumie upo katika dini zote.

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Naona watu wanapinga mafuta ya upako na wengine wakikubali.

Binafsi napinga utapeli unaofanywa na baadhi ya watu kwa kutumia dini .

Ila naomba nitoe ufafanui kidogo

Mwaka 2002 Babu yangu aliporudi Tanzania kutoka Saudi Arabia Macca katika mji wa Madina alikuja na maji Kama Lita tano hivi

Yale maji walipewa maujaji huko Macca (Madina) nakumbuka tulikuwa kila MTU anapewa kifuniko anakunywa

Yale maji yalikuwa tasteless -yapo Kama maji ya dukani tu Ila alituambia haya maji ni ya baraka.

Sasa kwa upande wa pili huwa wanakuaga na maji ya upako, mafuta n.k

Kinachotekea leo hii ni watu kutokuelewa maji ya upako yanapatikana vipi hii inaleta mkanganyiko na baadhi ya wajanja kupiga hela .


Kiufupi natoa ufafanuzi

Unaweza kuchukua maji ukayafanyia visomo then ukawa unayatumia katika ibada zako

Vilevile unaweza kuchukua mafuta ukayaombea na ukawa unayatumia katika ibada zako.


Je mafuta na maji yanaleta uponyaji ?

Ni swala la imani zaidi ukiamini kitu au jambo litakuwa.

na Kwa wale wanoamini mambo ya universe huwa wanatumia namba katika kumanifest mambo yao n.k is all about believe and faith.

ushauri

Viongozi wa dini mnaweza kuwashauri waumini wenu kuandaa mafuta au maji na kuyaombea wakawa wanatumia katika ibada zao kuliko kuwauzia.


Na mwisho MTU mwenye imani haitaji mafuta wala maji katika ibada zake.
 
Hakika ni suala la kiimani zaidi. Yote yanawezekana kwa imani
 
Back
Top Bottom