DOKEZO Utaratibu wa kupata Kitambulisho cha Taifa(NIDA) ni mgumu mno, Serikali iingilie kati

DOKEZO Utaratibu wa kupata Kitambulisho cha Taifa(NIDA) ni mgumu mno, Serikali iingilie kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Mwaka 2017 serikali ilileta utaratibu mzuri mno wa wananchi wa Tanzania kupata kitambulisho hiki muhimu cha Taifa

Iliendesha zoezi la kujiandikisha kuweza kupata vitambulisho hivi kila kijiji, na zoezi lilifanikiwa kwa zaidi za asilimia 70,kwani watanzania wengi walijiandikisha na kuweza kupata vitambulisho vyao,

Tangu zoezi hilo lisitishwe,hakuna tena zoezi lingine kama hilo,badala yake wananchi kulazimika kwenda wilayani (ofsi za nida) ili kuchukua au kupata hivi vitambulisho.

Lakini licha ya wananchi kulazimika kufanya bado wakienda huko huzungushwa sana mpaka wanakata tamaa, na katika ajira za serikali na sekta binafsi huwezi kupata kazi bila ya NIDA,hivyo wananchi wengi wanakosa ajira kwa kadhia hii.

Mimi kama mhanga wa jambo hili naiomba serikali yetu sikivu,inayojali vilio vya wananchi hasa wanyonge,waendeshe zoezi kama lile la mwanzo,ili wananchi ambao hawana nida wachukue kiurahsi ukilinganisha na hivi sasa,nadhan wale wanaohusika na NIDA waweke vituo vyao vijijini tuchukue NIDA zetu.

Thank you
 
Lengo lako mamluki kutoka Nchi jirani waje waingie humu kirahisi.
Haiwezekani vigezo vizingatiwe
Taratibu zifuatwe.
 
Lengo lako mamluki kutoka Nchi jirani waje waingie humu kirahisi.
Haiwezekani vigezo vizingatiwe
Taratibu zifuatwe.
imagine unatokea kijijini,unaenda ofsi za nida, mala unaambiwa utakuja kesho,ukienda kesho hivyo hivyo,hapo unatumia nauli,muda na huambulii kitu why zoezi lisifanyike kijijini tu watu wakachukua
 
Hao NIDA nao nikichefuchefu. Wanakusanya taarifa muda mrefu halafu kitambulisho wiki moja tu majina na taarifa nyingine zimefutika
Kitambulisho kinafutika maandishi kama risiti ya EFD Machine
Hii ni aibu
 
Lengo lako mamluki kutoka Nchi jirani waje waingie humu kirahisi.
Haiwezekani vigezo vizingatiwe
Taratibu zifuatwe.
Hapa Niko Bagamoyo na Kuna Mganda hapa kaandikishwa juzi cha kupigia kura kiurahisiii mpaka mwenyewe anashangaa.
Yaani yeye ametaja tu mji na Kijiji mpakani huko Kagera baassiii.
Anakwambia alikariri TU hicho Kijiji.
Intelijensia badi ipo ovyo
 
imagine unatokea kijijini,unaenda ofsi za nida, mala unaambiwa utakuja kesho,ukienda kesho hivyo hivyo,hapo unatumia nauli,muda na huambulii kitu why zoezi lisifanyike kijijini tu watu wakachukua
Hiyo haipo.
 
Back
Top Bottom