Jamani naombeni madini hapa mbona kimya?Mwajiri kaniachisha kazi bila kufanya haya,
1. Hajatoa nafasi ya kukata rufaa.
2. Hakutoa cheti cha utumishi.
3. Kamati ya kuchunguza tuhuma haikuwa
na kiongozi kutoka chama cha wafanyak
azi.
4. Kikao cha nidhamu kilifanyika nje ya
wilaya tukio lilipotokea.
5. Baada ya kikao cha nidhamu ilipita miezi
miwili ndipo akatoa barua ya termination
Je ni kipi kati ya hivyo siyo sahihi kwenye utaratibu wa kisheria?
Sijawahi pewa onyo lolote mkuuHayo yote uliyayaainisha yapo sahihi kama unlawful termination ila yatakuwa sisahihi kulingana na kosa ulilofanya, vilevile kama ulikwishapewa onyo kwa barua ama kwa mdomo kabla ya hiyo termination
Kosa ni kukusudia kuiba polisi wakachunguza wakaona sina kosa, barua ya polisi ninayo pia sijawahi pata onyo lolote kkNaomba kujua ulifanya kosa gani, je ulipewa barua ya onyo? Umesoma HR manual ya sehemu yako ya kazi inazungumzia nn kuhusu termination?
Ahsante mkuuMkuu Katus Manumbu
Hiyo namba 1 na namba nne pengine una hoja hapo.
Ila kesi yako ni rahisi ikiwa utapata Wakili mzuri maana ushasema kosa ni kukusudia kuiba na polisi wamechunguza wamekuta huna hatia na barua unayo ni hoja nzuri.
Kuhusu kukata rufaa, ulipaswa uonane na mwanasheria ili ikiwezekana umfungulie mashtaka muajiri wako.
Kufanya kikao cha nidhamu nje ya sehemu husika inaweza isiwe hoja endapo tu ulijulishwa kwa maandishi sababu ya kikao kufanyika huko.
Kesi yako ni rahisi kama tu utakuwa na nia ya dhati ya kupambana.
La zaidi inahitajika pesa tukusaidie kisheria.
Pesa wakati hana kazi mkuu!Mkuu Katus Manumbu
Hiyo namba 1 na namba nne pengine una hoja hapo.
Ila kesi yako ni rahisi ikiwa utapata Wakili mzuri maana ushasema kosa ni kukusudia kuiba na polisi wamechunguza wamekuta huna hatia na barua unayo ni hoja nzuri.
Kuhusu kukata rufaa, ulipaswa uonane na mwanasheria ili ikiwezekana umfungulie mashtaka muajiri wako.
Kufanya kikao cha nidhamu nje ya sehemu husika inaweza isiwe hoja endapo tu ulijulishwa kwa maandishi sababu ya kikao kufanyika huko.
Kesi yako ni rahisi kama tu utakuwa na nia ya dhati ya kupambana.
La zaidi inahitajika pesa tukusaidie kisheria.
Sijakuelewa kk
Huyo jamaa ni mtaalam wa sheria za kazi.Sijakuelewa kk
Sawa mkuuHuyo jamaa ni mtaalam wa sheria za kazi.
Mwajiri kaniachisha kazi bila kufanya haya,
1. Hajatoa nafasi ya kukata rufaa.
2. Hakutoa cheti cha utumishi.
3. Kamati ya kuchunguza tuhuma haikuwa
na kiongozi kutoka chama cha wafanyak
azi.
4. Kikao cha nidhamu kilifanyika nje ya
wilaya tukio lilipotokea.
5. Baada ya kikao cha nidhamu ilipita miezi
miwili ndipo akatoa barua ya termination
Je ni kipi kati ya hivyo siyo sahihi kwenye utaratibu wa kisheria?
Ndiyo tuhuma ni kukusudia kuibaBarua ya termination inasema umefukuzwa kazi kwa sababu ya kukusudia kuiba? Maana wasije wakasema wamekufukuza kwa sababu nyingine.
Hakuna wizi uliotokea kkKosa ni kukusudia kuiba au wizi umetokea kikwelikweli na wewe ukawa mtuhumiwa? Weka wazi kila kitu ili usaidiwe mawazo kwa usahihi
1.Niliambiwa ila kikao kilipelekwa wilaya nyingine nikashindwa gharama za kupeleka mashahidi.1) Katika kikao cha nidhamu uliambiwa ulete shahidi wako? Na ulifanya hivyo?
2) Uliwahi kutuhumiwa kwa kosa lolote kabla ya hilo? Yani una BARUA YA ONYO ambayo uliwahi kupewa? Au ONYO ya mdomo na mwajiri wako? Au uliwahi kukutwa na hatia kabla hapo kazini na kosa lolote lile?
3) Hasara uliosababisha kwa huyo mwajiri wako, ulikatwa kwenye mshahara au ulilipishwa?
4) Kosa ulilofanya ni JINAI (wizi n.k) au ni UZEMBE KAZINI uliosababishia kuachishwa kazi?
Pia weka wazi kosa lililosababisha wewe kufukuzwa, kumbuka ni vyema ukawa mkweli kwetu, kwani ukitudanganya sisi tutaishia kukupa ushauri kutokana na kauli yako usio na mashiko, mwisho wa siku itakua ni kazi bure maana mwajiri wako atakuja na ushauri wenye mashiko.
Ushauri wa kesi sio kama ushauri wa kuuza nyanya au bamia, unapaswa kua mkweli kabisa, ili watu wajue wanakushauri vipi.
Nafasi bado unayo ya kukata rufaa;
1) Mediation & Arbitration centre (Labour Court).
2) High Court Labour Division.
Kama ni hivyo ulivyoelezea katika maelezo yako, basi mwajiri amekuonea na haki yako unaweza ukaipata (nakushauri tafuta mwanasheria akusimamie swala lako ili iwe rahisi kupata haki yako, ila kama utaweza kujisimamia mwenyewe pia sawa). Kuna njia mbili unaweza ukatumia;1.Niliambiwa ila kikao kilipelekwa wilaya nyingine nikashindwa gharama za kupeleka mashahidi.
2.Sijawahi fanya kosa wala kupewa onto lolote.
3.Hakuna hasara yoyote iliyosababishwa.
4.Ni kosa la jinai (kukusudia kuiba).
Kesi ilikuwa hivi;
Nilikaimishwa nafasi 2 za uongozi, kama meneja pia mkuu wa idara. Likaja gari la mafuta invoice na delivery note za mzigo zinaonyesha Lita 15,000. Kihualisia mafuta yaliyokuwa ndani ya tanker la gari ni Lita 18,000 ambapo kiasi cha Lita 3,000 zikawa zimezidi.
Nikapokea mafuta Lita 15,000 kama documents zilivyosema na kuacha Lita 3,000 zilizokuwa zimezidi zirudishwe zilipotoka kama dereva alivyokuwa amesema, nikaandika barua kuelezea jinsi ilivyokuwa na nilichokifanya. Gari likaondoka kufika wilaya jirani likakamatwa na polisi, likarudishwa lilipotoka kesi ikaanzia hapo.
Wakaja watu kuchunguza hawakukuta upungufu wowote wa mafuta kisha Jeshi la polisi nao wakafanya uchunguzi na wakaona sina hatia kwa kuwa ktk mali ya Mwajiri hakuna loss yoyote. Hivyo tuhuma ya wizi haipo. Polisi waliandika barua kwenda kwa mwajiri na kusema kwamba hawaoni kosa langu.
Mwajiri yeye akaamua kunichukulia hatua za kinidhamu na kuniachisha kazi.
Naombeni mawazo yenu hapa.