Kama ni hivyo ulivyoelezea katika maelezo yako, basi mwajiri amekuonea na haki yako unaweza ukaipata (nakushauri tafuta mwanasheria akusimamie swala lako ili iwe rahisi kupata haki yako, ila kama utaweza kujisimamia mwenyewe pia sawa). Kuna njia mbili unaweza ukatumia;
Njia ya kwanza, mwanasheria waki amwandikie barua muajiri wako (DEMAND NOTICE) kumuamuru akulipe fidia mtakayoitaka ndani ya siku mtakazompa (either siku 14 au 21 au zaidi), akimalizia kwa onyo kua asipotimiza maombi yenu ndani ya hizo siku basi mtamchukulia hatua kali za kisheria dhidi yake. (TAMBUA barua hii lazima iwe imeandikwa kisheria kwa kuchambua makosa aliofanya mwajiri, ushahidi uliopo dhidi yake, na ushahidi wa hasara uliopata ili iwe na nguvu).
Njia ya pili,
1) Andaa vithibisho na document zote za ushahidi (copy na original). ***Hio barua ya Police ni muhimu sanaa uwe nayo.
2) Kafungue madai ya UNFAIR TERMINATION katika mahakama ya kazi.
Maombi yako mbele ya mahakama unaweza ukaomba;
i) Mahakama ITOE TAMKO/TAFSIRI/HUKUMU kua umefukuzwa kazi kwa uonevu/kinyume na sheria/bila kufuata utaratibu wa sheria za kazi.
ii) Pili, kumshtaki mwajiri kwa kukufukuza kazi bila uhalali/kufuata sheria na kudai fidia unayoitaka kutokana na hasara ulizopata kwa kufukuzwa kazi (mfano mshahara wa mwaka mmoja/hasara za fedha ulizo/utakazomlipa mwanasheria wako/hasara za kuendesha kesi mpaka iishe/na gharama nyingine).
Ushauri wangu tafuta mwanasheria/wakili akusaidie.