Kirchhoff
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,735
- 8,541
Nimekuwa nikifuatilia matukio mbalimbali ya Kiserikali na kijamii mara nyingi. Niseme tuu Sipendwezwi na Utaratibu Wa Kutaja na kutambuana Viongozi kabla ya kuanzia hotuba au salamu zao.
Mfano Leo Hapa Arusha, Jukwaa kuu Lina Viongozi Zaidi ya Ishirini na Kila kiongozi anayetaka kuongea analazimika Kutaja na kutambua Viongozi wote waliopo.
Kiongozi anatumia dakika Tano Kutaja Viongozi waliopo ambao tena watatajwa na Viongozi wengine wanaofuata.
Ni Kwa Nini kusiwe na Mtaja ITIFAKI Mmoja Tuu Mwanzoni atambue uwepo wa watu wote? Kisha Kila Mtoa Hotuba amtaje tuu Mgeni Rasmi labda na Mwenyeji wake na pia Mgeni Rasmi pia katika hotuba yake atambue uwepo wa hao watu katika hotuba yake.
Hii itaondoa uchovu wa kusikiliza marudio ya Majina na vyeo vya Viongozi waliohudhuria jambo Husika.
Wakati wa Maghufuli Mwanasayansi Mbobevu alizingatia Mda na mara nyingi hakutaka watu warudie rudie kutajanatajana hovyo.
Nawasilisha.