Mkuu samahani sana siwezi kukosea kukupa taarifa kwa sababu kadhaa nina experience na hii kitu
Nishawahi kutoa taarifa kwa rpc kuhusu bis kujaza abiria, mwisho wa siku mwwnye bus akatumiwa namba naye akaituma kwa konda, konda akaanza kunitafuta baada ya kup8gwa fine, ilibidi niteremkie njiani robo ya safari coz nlikuwa natoka mwanza naenda musoma, jamaa walikuwa wanaseme tukikupata tunakukata mapanga.
Wewe sikujui naweza kukupa taarifa ndo nikaharibu hadi mahusiano na jirani yangu ambaye ndo kishoka wao
2. Hawa watu wana familia nikiwachoma wakafukuzwa kazi familia zao zitateseka.
Kwa taarifa hii jaribuni kuweka usimamizi mzuri wa mjukumu yenu ila sio kushughulika na tatizo langu peke yangu. Naamini kuna watu wengi wanapatwa na shida kama yangu hawana pa kusemea.