Utaratibu wa kutoa talaka upoje?

Maisha ni mepesi ssna,wenzetu mnacomplicate sana maisha,talaka nipeleke mahakaman kwan wao ndo waliniozesha??talaka natoa mm wengine nawqpa taarifa tu kuanzia leo fulani siyo mke wangu basiii,siyo naendw kuwaomba ruhusa ya kumuacha as if wanaishi naye wao!!
 
Kwa ufafanuzi huu mzuri,ndugu mleta mada unasemaje. Ujipangee au ukimbie tu huo msala?
 
Wewe jamaa kwenye mijadala isiyo ya kisiasa una akili sana
 
Nimeufata ushauri wa bwana Mideko reply #15
Safi sana. Ili uwe huru ni vizuri kufanya hivyo. Hawa wanawake zetu pasua kichwa sana mkuu. Wengi wetu tunachagua kuishi nao ili mradi tu maisha yaende. Wanachochea sana uzinzi tunajukuta una mademu wa kupiga nje kutafuta furaha
 

❌ Kwa Sheria ya ndoa ya Tanzania , hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuandika Wala kutoa talaka tofauti na Mahakama baada ya kupitia taratibu zote na kubaini kuwa ndoa imevunjika vipande vipanda Haina spea na Wala haitawezekana tena kwa wanandoa hao kuishi pamoja.

✅ Utaratibu, unasnzia kwa Baraza la usuluishi la Kata, pale ambapo mmoja wa wandoa ataoeleka malalamiko, basi Baraza litawaita na kuwasikiliza kwa lengo sii la kuvunja ndoa Bali kuwasuluisha maana kwa mujibu wa kifungu Cha 9 Cha Sheria ya ndoa na kesi ya Hyde vs Hyde lengo la ndoa ni wanandoa waishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe. Baraza likishindwa kusuluisha litaandika certificate kwa mahakama kuwa usuluishi umeshindikana. Hivyo hakuna kesi yoyote ya maombi ya talaka yatapikelewa mahakamani kabla ya kupitia kwenye Baraza la usuluishi linambulika kisheria. Mtu mwenye dini Fulani ambapo ndoa imefungwa kwa misingi hiyo na wanayo mabaraza ya usuluishi, mabaraza hayo yanaweza kutbulika kama mbadala wa mabaraza ya Kata.

✅ Kesi ikifika mahakamani, baada ya kuwasikiliza itsona kama kweli haiwezekani wanandoa Hawa kuendelea kuishi pamoja na kabla haijatoa talaka lazima itoe muda wa kisheria wa wanandoa kujitafakari hii order ni separation ambayo ni decree nisi.

✅ Baada ya muda wa separation kuisha mahakama itawasikilizs tena kama bado mambo ni magumu basi itatoa talaka na amri za matunzo ya watoto ( kama wapo) na mgawanjo wa Mali walizochuma pamoja .

❌ Hivyo, kwa Sheria zetu, makatatasi wanaojiandikia watu kwa kusema mara ni talaka tatu, mara talaka rejea kimsingi Yale sii talaka na hayana effect ya kuvunja ndoa, mmoja wao akienda mahakamani kesi inasikilizwa upya kwa mujibu wa Sheria na haki inatolewa. CHOMBO CHENYE MAMLAKA YA KUVUNJA NDOA KISHERIA TANZANIA NI MAHAKAMA TUU
 
Kwani mungu yeye aliwahi kuoa,
 
Safi sana. Ili uwe huru ni vizuri kufanya hivyo. Hawa wanawake zetu pasua kichwa sana mkuu. Wengi wetu tunachagua kuishi nao ili mradi tu maisha yaende. Wanachochea sana uzinzi tunajukuta una mademu wa kupiga nje kutafuta furaha
[emoji419][emoji419][emoji419]
 
Ungemquote mtoa mada sio mimi.
Mimi nafahamu taratibu zote
 
Ha ha ha watu wanashidwana kisha wanamsingizia Mungu.
Kama ulikuwa unafahami Sheria ya nchi inasemaje kuhusu talaka, na kama unafahamu mamlaka yenye nguvu ya kisheria kutoa talaka sii kanisa, msikiti au muoaje ungemshauri afanye kwa mujibu wa Sheria akaanzie kwenye ( marriage conciliation board) ili apate certificate ya kwenda mahakamani, na Mahakama iangalie kama zile elements za kwamba marriage has broken down irreparably zimetimia na hivyo kutoa talaka ambayo itawaacha huru
 
Uko sawa ninachopinga ni kumwachia mungu.
 
Kuna mtu katumia ID yako kuandika huu ujumbe? Maana haiwezekani kabisa kwamba ni wewe!
 
Closed wapi wewe?

Mwanaume kushindwa kuishi na mke ni wazi kuwa huyo mwanaume akili hana
Asiye na akili haruhusiwi kufungua kesi ya talaka

Ungeshauri mwanaume akapimwe akili kwanza hospitali ya vichaa mirembe
Wewe unatakiwa upelekwe mirembe, kwa komenti hizi naamini dishi limeanza kuyumba.
 
Sio rahisi Kama unavyo dhani ndoa Ni Mali ya serikali
 
Mbona baadhi ya watu mnapenda ndoa iwe ni kitu cha kung'ang'aniana hata kama mmeshachukiana? Kwa sababu ya nini sasa muishi kwa mateso na kuvumilia?
 
Mkuu next time andika Kwa paragraph maana jinsi ulivyoandika inatia hata uvivu kusoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…