Utaratibu wa kuwahamisha watumishi wa umma idara ya afya halmashauri ya mji Masasi mtwara kuwapeleka Sekta Binafsi uangaliwe upyaa

Utaratibu wa kuwahamisha watumishi wa umma idara ya afya halmashauri ya mji Masasi mtwara kuwapeleka Sekta Binafsi uangaliwe upyaa

boy lanugo

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2015
Posts
290
Reaction score
272
Fikiria unawapelekea Vituo binafsi vijana wenye nguvu, kisa wanahoji kuhusu matumizi ya hela ambazo ki msingi wao ndio wanazikusanya? Kituo cha private unapeleka wafanyakazi zaidi ya wawili hapo nani ananyfaidi?
Serikali inafaidikaje na hawa watumishi waliopo vituo hivi?

Unamtoa Mfamasia unampeleka kituo binafsi bila kazi yoyote ile ya kufanya .kituo alichopekekwa hakina hata store maskini ya mungu, hasimamii chochote kwani private ni biashara zaidi na si huduma.

Halafu unaacha madirisha ya dawa ya hospital ya wilaya yakiendeshwa na Medical attendant kweli. Ukifika duka la MSD la hospital ya wilaya unakutana na hawa wanaovaa nguo za kijani ndio wanasimamia duka je ni sahihi?

Mbaya zaidi mtumishi anahamishwa halipwi hata stahiki zake , kila akiomba anaambiwa utalipwa andika barua unaandika na kesho unahamisha tena .

Kuna mfanyakazi kahamishwa vituo 4 ndani ya miaka 4 ni haki kweli?
Kuna haja ya kuangaliwa upya namna ya kuhamisha watumishi. Zisitumike chuki binafsi na husda za roho mbaya huku kaZi za serikali zikikwama
 
kwani sekta binafsi wanahudumiwa mbuzi??
 
Back
Top Bottom