Utaratibu wa kuwakata Wapangaji hela kila wanaponunua umeme, unauma sana

Utaratibu wa kuwakata Wapangaji hela kila wanaponunua umeme, unauma sana

Michael mbano

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2022
Posts
820
Reaction score
570
Huu utaratibu wa kuwakata hela yao wapangaji wanaponunua umeme unawatesa wapangaji, kwa kuwa wananchi wapole na wanalia na machozi yanaishia ndani ndiyo mana hamjali?

Juzi nilikuwa nanunua umeme wa Tsh. 5,000 ukagoma, nikaongeza wa 1,000 ukagoma. Nikaweka 12,000 ndipo wakakubali tena umeme wa 2,000 tu ile 10,000 wakalamba inaniuma.

Wahusika mliangaliye hili.
 
Huu utaratibu wa kuwakata hela yao wapangaji wanaponunuwa umeme unawatesa wapangaji,kwakuwa wananchi wapole na wanalia na machozi yanaishia ndani ndiyo mana hamjali?Juzi nilikuwa wananunuwa umeme wa5000ukagoma,nikaongeza wa 1000 ukagoma.Nikaweka 12000ndipo wakakubali tena umeme wa2000tu ile 10000 wakalamba inaniuma.Wahusika mliangaliye hili.
Michael mbano unachofanya ni kama swala kwenda kando ya mto na kuwaambia mamba ''jamani tunaomba mliangalia hili suala la kutufanya kitoeo wakati tunapokuja kunywa maji''. Unadhani mamba watajibuje? Ukweli mchungu: bila wananchi kujitambua na kuanza kuiadabisha serikali na viongozi wake bila woga, ikiwezekana kukinukisha wakinukishe, hakutakuwa na mabadiliko!
 
Tumeyapokea tutayafanyia kazi kwenye Loyo tua. BTW hata marekani wanakatwa
 
Watanzania tunaongea sana bila vitendo,na hilo viongozi wa serikali wanalijua hivyo wanaamua tu wanavyotaka,
Na maamuzi mengine wamekuwa wakiyatoa wakiwa mahotelini na wapenzi wao,haiwezekani mtu kapanga alafu unamkata kodi ya majengo kupitia umeme anaonunua
 
Michael mbano unachofanya ni kama swala kwenda kando ya mto na kuwaambia mamba ''jamani tunaomba mliangalia hili suala la kutufanya kitoeo wakati tunapokuja kunywa maji''. Unadhani mamba watajibuje? Ukweli mchungu: bila wananchi kujitambua na kuanza kuiadabisha serikali na viongozi wake bila woga, ikiwezekana kukinukisha wakinukishe, hakutakuwa na mabadiliko!
Kweli usemalo.Inauma sana waTZ tufike mahala tuungane tuseme tosha bidhaa nyingi tununuazo zimeunganishwa na kodi lakini bado tu jaman .Huku tozo za miamala,huku luku mwee
 
Nchi ninayoishi mimi kuna kodi kama 9 hivi kwenye bili ya maji na umeme. Barabara ni nzuri na pesa nyingine huja huko kama misaada. Zikienda kwenye kuchangia maendeleo siyo shida.
 
Huu utaratibu wa kuwakata hela yao wapangaji wanaponunua umeme unawatesa wapangaji, kwa kuwa wananchi wapole na wanalia na machozi yanaishia ndani ndiyo mana hamjali?

Juzi nilikuwa nanunua umeme wa Tsh. 5,000 ukagoma, nikaongeza wa 1,000 ukagoma. Nikaweka 12,000 ndipo wakakubali tena umeme wa 2,000 tu ile 10,000 wakalamba inaniuma.

Wahusika mliangaliye hili.
Hiyo mita itakuwa ina deni,mnakaa chini na mwenye nyumba kuangalia namna ya kufidia hizo pesa.
 
Mpeni pesa mwenye jengo awe ananunua mwenyewe
 
Siyo ile kodi ya nyumba ambayo serikali iliingiza kwa wapangaji kibabe?Yani serikali inajuwa sisi kama mnyama achinjwaye atarusha mateke na kutetemeka halafu atatulia duh!.
 
Watanzania tunaongea sana bila vitendo,na hilo viongozi wa serikali wanalijua hivyo wanaamua tu wanavyotaka,
Na maamuzi mengine wamekuwa wakiyatoa wakiwa mahotelini na wapenzi wao,haiwezekani mtu kapanga alafu unamkata kodi ya majengo kupitia umeme anaonunua
INAUMIZA SANA MWENYE NYUMBA ANACHUKUWA PANGO KWA MPANGAJI YE NDIYO AKALIPE KODI YA JENGO SIYO WAPANGAJI.MAMBO HAYA NDIYO HUCHOCHEA HASIRA DHIDI YA SERIKALI.
 
Back
Top Bottom