Utaratibu wa kuwaunganisha Watanzania na ajira nje ya nchi warejeshwa

Utaratibu wa kuwaunganisha Watanzania na ajira nje ya nchi warejeshwa

Bright eyes

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2021
Posts
228
Reaction score
303
Jamaa nchi inazidi kufunguliwa hukuu. Fursa hiyoo kwa watafutaji.

Wale mawakala wa dubei, Qatar n.k na wale watafuta kazi nje ya nchi mambo yamenoga huku.

Mimi nataka nikafanye zangu kazi dubei, nimechoka kupambana na wachina na wahindi wa Bongo 😁😁

Habari Kamili 👇👇👇👇

========

SERIKALI imerejesha utaratibu wa kuwaunganisha Watanzania na ajira nje ya nchi kuanzia juzi.

Taarifa iliyotolewa juzi jioni na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ilisema serikali imerejesha utaratibu huo ili kutoa fursa kwa watanzania wenye shauku na sifa kufanya kazi nje ya nchi.

“Kwa kutambua mchango mkubwa wa fursa za ajira zinazopatikana nje ya nchi katika maendeleo ya nchi yetu, na kwa kuzingatia kuwa, tunao Mwongozo kwa Mawakala Binafsi unaobainisha masuala ya msingi katika kuunganisha watanzania na fursa za ajira nje ya nchi.

“ Tunapenda kuufahamisha umma wa Watanzania hususani Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira pamoja na Watanzania wenye shauku na sifa ya kufanya kazi nje ya nchi kuwa, shughuli za kuunganisha Watanzania na fursa za ajira nje ya nchi kupitia Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira zinarejeshwa rasmi kuanzia leo (juzi) kwa kuzingatia Sheria, Kanuni pamoja na Mwongozo Mpya.”

Julai 2018, Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi na ajira alisitisha huduma ya kuunganisha Watanzania

na fursa za ajira nje ya nchi kupitia Mawakala Binafsi wa Huduma za Ajira. Hatua hii ilitokana na ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni uliokuwa ukifanywa na baadhi ya Mawakala.

Pia Serikali ilichukua hatua hizo ili kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha Watanzania kunufaika zaidi na fursa za ajira nje ya nchi.

“ Hivyo basi, tunawajulisha Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini ambao wamepata fursa za ajira kwa Watanzania nje ya nchi kuwasilisha maombi yao kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ajira (TaESA) ili waweze kupatiwa vibali vya kuunganisha watanzania na fursa husika” ilisema taarifa hiyo.

Aidha, Serikali imesema inatambua na kuzingatia kuwa katika kutumia fursa za ajira nje ya nchi usalama na haki za msingi kwa Watanzania ni suala lisilo na mbadala na hivyo ni lazima uunganishaji wa watanzania na fursa za ajira nje ya nchi uzingatie viwango vya kazi za staha vinavyokubalika na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Taarifa hiyo imesema kwa wale wasio na leseni na wana fursa za ajira nje ya nchi wawasilishe maombi ya leseni kwa Kamishna wa Kazi yakiambatana na ada ya usajili ya kipindi cha mwaka mmoja isiyorudishwa kiasi cha Sh 500,000.

Source : Habari Leo . Jan 2 2022
 
Duh kumbe walizuia??Ili iweje??
Heee!!walizuia kipindi kile kangi lugola akiwa waziri wa mambo ya ndani, eti naenda kutafuta nini wakati kila kitu kipo nchi!!!ili kupita uwanja wa ndege ilikuwa inshu ukiwa eti unaenda kufanya kazi nje!!tumepitia kipindi kigumu sana 2016-2020!!tulikuwa tunaenda kuwa N.KOREA.
MUNGU FUNDI.
 
Mimi nimetembea sehemu tofauti tofauti ndugu zanGu lakini nilichokuja kugundua KWA HAPA DUNIA HAKUNA SEHEMU NZURI KAMA TANZANIA NA KENYA.

Nchi hizi mbili zimejipatia sifa kubwa hasa huko DUNIA SAFI

Tutafute maarifa tu ili tuijenge afrika
Sasa kama ulitembelea burundi drc sauzi sudani ni kwanini usione bongoland na Kenya ndo pepo?
 
Heee!!walizuia kipindi kile kangi lugola akiwa waziri wa mambo ya ndani, eti naenda kutafuta nini wakati kila kitu kipo nchi!!!ili kupita uwanja wa ndege ilikuwa inshu ukiwa eti unaenda kufanya kazi nje!!tumepitia kipindi kigumu sana 2016-2020!!tulikuwa tunaenda kuwa N.KOREA.
MUNGU FUNDI.
kuuumbe wewe ndo hukujua sasa!!! wenzako hapo hapo ndo walipo kazia!! na ndo tulichomokea hapohapo! bila kuchelewa ndo ilikuwa fursa ile!!.... mpaka ma Boss wetu wakaduwaa na ku tupachika majina OOOh!! yule smaki Usalama wa Taifa kaondokaje na yeye ni mtumishi wa Umma???

Wengine walikuwa wanaondoka usiku na Rwanda air ways!! wkt maafisa usalama wamechoka Lindoni!! wamelala au unagongewa wakiwa na usingizi mziito yaani unaweza cheka!... nikaamini dooo!!! kweli Bindamu hachungwi bana weee!!
 
Nasikia kuna mdada wa kiganda katolewa figo huko baadhi ya waarab sio watu wazur kabisa
 
Ila yule mla michembe wa burigi sijui alikuwa anataka tuishije hakika acheni Mungu aitwe Mungu

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kmmk na hilo pori sijui kama linaendelezwa
 
kuuumbe wewe ndo hukujua sasa!!! wenzako hapo hapo ndo walipo kazia!! na ndo tulichomokea hapohapo! bila kuchelewa ndo ilikuwa fursa ile!!.... mpaka ma Boss wetu wakaduwaa na ku tupachika majina OOOh!! yule smaki Usalama wa Taifa kaondokaje na yeye ni mtumishi wa Umma???

Wengine walikuwa wanaondoka usiku na Rwanda air ways!! wkt maafisa usalama wamechoka Lindoni!! wamelala au unagongewa wakiwa na usingizi mziito yaani unaweza cheka!... nikaamini dooo!!! kweli Bindamu hachungwi bana weee!!
Mimi nilimanisha kuwa kwa tamko la serikali walizuia, sasa hayo mengine yapo tu, hata leo hii kila leo kuna matamko ya rushwa kuwa ni marufuku kwani watu hawapokei?!!
 
Mimi nilimanisha kuwa kwa tamko la serikali walizuia, sasa hayo mengine yapo tu, hata leo hii kila leo kuna matamko ya rushwa kuwa ni marufuku kwani watu hawapokei?!!
Mpaka leo hii nasema hakuna anae kula rushwa katu!! kwa sababu tumelikataa hili kitambo kuwa rushwa ni adui wa haki!!! km unakula ni wewe wa kukushughulikia!! wapi umeona rushwa Bongo??? sema wapi??? nikujibu saa hivi ...
 
Back
Top Bottom