Utaratibu wa kuzuia magari kwenye misafara ya viongozi ubadilike

Utaratibu wa kuzuia magari kwenye misafara ya viongozi ubadilike

JFMemba

Senior Member
Joined
Jun 28, 2021
Posts
134
Reaction score
247
Leo sijui kiongozi gani alikuwa na ziara ipi mi sijui lakini kile kitendo cha kuwekwa saa mzima Ubungo pale tunasubiri mtu mmoja apite ni kaushamba sana.

VIONGOZI hawaoni kwamba hii ni kero kwa wananchi, wewe hayo unayoyafanya ndio yanakupa ulaji, pengine hata usipofanya ziara mshahara utapata tu. Kutuzuia sisi wengine ambalo kipato chetu kinatokana na mihangaiko na mishe za hapa na pale sio poa.

Kupoteza saa moja hujui nilikuwa nawahi dili gani inashusha uchumi. Yani tumekosa kabisa alternative ya hili? Wahurumieni wananchi bana.
 
Tuseme daktari bingwa anawekwa kwenye foleni kwa ajili ya msafara, wagonjwa watakufa sababu ya mtu mmoja. Waende Sweden wakaone misafara ya viongozi ili wajifunze.
 
Leo hapa Morogoro masaa mawili gari zimesimamishwa
 
Back
Top Bottom